Profesa Kitila Mkumbo kamaliza kuhusu elimu Tanzania

Profesa Kitila Mkumbo kamaliza kuhusu elimu Tanzania

Teleza1

Senior Member
Joined
May 16, 2020
Posts
190
Reaction score
198
Pro kitila leo kamwaga nondo za kufa mtu ushauri wake serikali ikiuzingatia tutafika mbali sana.
Ukianza na degree ya ualimu iwe miaka minne for freshers Yaaani form six na diploma iwe miaka 3 ni wazo zuri kwanza itandoa mrundikano wa wanaopanga foreni kusubiria ajira kwani miaka itakuwa mingi ya kuhitimu mafunzo.

Pia itatusaidia kupata waalimu competent katika masomo yao. Kwani mwaka mmoja wa kukaaa mashuleni utawasaidia kujua na kuongeza maarifa kwa kile wanachoenda kukifundisha. Lakini msisitizo mkubwa uwekwe upande wa shule za msingi kwani hali ni mbaya watoto hawajui kusoma wanafanyiwa mitihani.

Pili waalimu kupewa posho utaaratibu ungeanza mara moja hususani kwa waalimu wa hisabati na kuingereza kwakua huko bado ni majanga makuwa sana waalimu wa kiingereza na hisabati wangepewa kipaumbele cha posho. Unaweza kuta mwalimu anafundisha hesabu kuanzia form one mpk 4m4.halafu ingekuwa ni motisha hata kusaidia kuongeza waalimu wa hesabu.

Chama cha waalimu CWT kimekuwa kinalalamikiwa sana yaaani hawa ni wezi waliohalalishwa yaaani wenyewe kazi yao ni kutata watu nishahara tuuuu mfano mwaka huu hata gawio tsheti hawajatoa lakini kazi yao nu kukata waalimu mishahara.hawa ni wezi hiki chama kifutwe watu warudishiwe michango yao .

Maafisa elimu kata hiki cheo kifutwe ni cheo ambacho kinaigharimu serikali mabilioni ya pesa na na kupunguza nguvu kazi mashuleni kuns afisa elimu kata nilimshuhudia anafanya kazi songea anaishi njombe yaaani hawa hawana kazi wanaitia serikali hasra na kupunguza nguvu kazi mashuleni.

Kuna ofisi moja ya elimu nilienda nikakuta ina watumishi ( waalimu ) zaidi ya 30 tena wakabila moja na wanaongea kilugha full na hawa kusikilizi ukiwa sio wa kabila lao sasa hawa wote wakirudishwa kufundisha itaongeza nguvu kazi mashuleni.serikali ipunguze pia watu waliojsza mademu zao halmashauri.Kuna zoezi la sensa hivi watajazana wenyewe kama wasimamizi wa maudhui na tehama wanakera sana.

Elimu bure ni janga kwa serikali wazazi wachangie elimu za watoto wao.

Ushauri wa kitila mkumbo ukizingatiwa utaleta matunda chanya
 
Back
Top Bottom