JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema katika miaka 25 ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo (2000-2025) kiwango cha umasikini kimepunguzwa hadi kufikia asilimia 26, na lengo ni kumaliza katika miaka 25 ijayo.
Profesa Mkumbo amesema hayo katika kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC1 kutoka jijini Dodoma kuelekea bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka 2024/25 ambayo itawasilishwa bungeni Juni 13, 2024.
"Kama tumeweza kupunguza hadi kufikia asilimia 26, tunataka kuona hii asilimia 26 kuelekea mwaka 2050 tuweze kuondoa kabisa," amesema Profesa Mkumbo huku akiongeza kuwa suala la kuondoa umasikini ni la nchi zote duniani kwani hakuna nchi iliyofanikiwa kwa asilimia 100.
Ameongeza kuwa utekelezaji wa dira inayofikia ukomo mwaka 2025 umekuwa na mafanikio makubwa pamoja na changamoto mbalimbali.
"Mwaka 2000 hali ya upatikanaji wa maji vijijini ilikuwa asilimia 32, lakini sasa tunazungumzia asilimia 79.8, karibu asilimi 80. Kwa hivyo utaona kazi kubwa ambayo imefanyika katika miaka hii 25," amesema Profesa Mkumbo.
Kwenye sekta ya elimu amesema mwaka 2000 chini ya asilimia 10 ya waliomaliza shule ya msingi ndio walipata fursa ya kwenda sekondari, lakini sasa kati ya wanafunzi 100, wanakwenda sekondari wanafunzi 70, takwimu zinazothibitisha kuwa kazi kubwa imefanyika.
Amesema kuwa sasa Serikali inaandaa dira ya miaka mingine 25 ijayo (2025-2050) na sasa ipo katika hatua ya kukusanya maoni ya wananchi juu ya mambo wanayotaka yajumuishwe kwenye dira hiyo, na hivyo amewasihi wananchi wa makundi yote kujitokeza kutoa maoni yao.
"Tunataka kufika 2050 iwe ni uchumi wa kati juu, maana yake ni kwamba hakuna Mtanzania yuko chini ya kiwango cha chini cha umasikini," ameongeza.
Chanzo: TBC 1