Uchaguzi 2020 Profesa Lipumba: Mkinichagua kuwa Rais wa Nchi hii nitafuta umasikini katika nyanja zote

Uchaguzi 2020 Profesa Lipumba: Mkinichagua kuwa Rais wa Nchi hii nitafuta umasikini katika nyanja zote

CUF Habari

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2019
Posts
239
Reaction score
234
Screenshot_20200909-183500.png


MKINICHAGUA KUWA RAIS WA NCHI HII NITAFUTA UMASIKINI KATIKA NYANJA ZOTE "PROF.LIPUMBA" AKIWA BAGAMOYO​

Ukuaji wa uchumi wa Tanzania haujaambatana na kasi kubwa ya kupungua kwa watu masikini. Idadi ya watu masikini kwa kutumia kipimo cha taifa cha umasikini (mtu mzima kutumia shilingi 50,000/ au zaidi kwa mwezi) imeongezeka toka watu milioni 12.3 mwaka 2011 na kufikia watu milioni 14 mwaka 2018. Kwa kutumia kipimo cha kimataifa cha umaskini, Watanzania zaidi ya milioni 27 ni masikini.

Utafiti uliofanywa na Serikali mwaka 2016 kuhusu umaskini wa watoto (Child Poverty in Tanzania) ulibaini kuwa asilimia 74 ya watoto wa Tanzania wanaishi katika mazingira ya umaskini kwa tafsiri pana inayojumuisha lishe, afya, hifadhi iliyo salama, elimu, mazingira, maji na makazi.
 
Back
Top Bottom