Kwanza napenda kukupongeza wewe binafsi kwa kuwa nakuona unajitahidi sana kujaribu kuleta suluhu kwenye suala la ubora wa elimu yetu.Hata hivyo jitihada zako pamoja na washauri wako bado hamjaweza kutatua kiini cha tatizo ambalo kimsingi sisi wadau wengine tunaliona.
Mimi sina elimu kubwa lakini nitajaribu kuongea vitu vichache kwa mifano halafu ninyi wabobezi na maguru mjaribu kuyaweka katika muktadha wa kisomi.
Wanafunzi wengi wanafeli kwa kuwa kuna vitu havileti mvuto kwa vile hata ukivijua havina mantiki wala msaada wowote kwenye maarifa (skills)
Mfano unamfundisha mtoto kuandika hatua tano za kuendesha baiskeli. Unamuuliza kwenye mtihani akuekeze hatua hizo tano.
Majibu uliyo nayo kuna watu waliandika na kwa hiyo unamkaririsha mtoto ajibu kama walivyofikiri wengine.
Mtoto huyu ambaye kila siku anakuja shuleni akiendesha baiskeli,anashindwa kujieleza hizo hatua unazotaka aziandike kwa mujibu wa majibu uliyonayo,wewe unasema hana akili ila yeye anajua kuendesha baiskeli pasipo kusoma hizo nadharia zako.
Au una mwanafunzi unataka ajue kushona nguo kwa kutumia cherehani,unachukua miaka miwili unamfundisha hesabu za maumbo,unamfundisha fizikia ya cherehani,kisha unampima kwa hayo ukitaka upate fundi wa ushonaji mahiri.
Hii ni kupoteza muda kwani kujua fizikia ya cherehani sio jukumu la msingi la fundi wa ushonaji ingawa sio vibaya kujua.
Au kujua fizikia ya baiskeli, na kwa nini mwendeshaji ana balance kwenye tairi mbili,sijui akienda spidi kubwa balansi inakuwa thabiti au akienda spidi ndogo anatumia nishaji ( energy) kubwa ama ndogo hivi vitu sio vya msingi kwa mwendesha baiskeli.
Elimu inapsawa kuchuja nini cha kusoma kwa lengo gani.
Elimu yetu ilivyo ya kijinga,ni kama unamuona mchezaji kama Messi amecheza mpira kwa umahiri sana,kisha akaandika kitabu jinsi ya kucheza mpira vizuri ,sisi tunatumia muda mwingi kwenye nadharia ya jinsi ya kucheza mpira vizuri halafu tunatarajia mtoto aliyepata alama nyingi, acheze kama Messi.
Huu ni zaidi ya upumbavu. ( Shukrani Messi hajaandika kitabu) maana watoto wetu wangehenyeshwa na nadharia za hizo ili Wawe wachezaji bora.Kumbe tunaandaa wachambuzi wa soka badala ya wachezaji wa mpira.
Elimu yetu kwa kiasi kikubwa inaandaa wachambuzi wa maarifa na sio watendaji wa maarifa.
Katika nyanja nyingi tuna wachambuzi wa taaluma badala ya wataalamu.
Wamekariri majibu kuhusu taaluma zao lakini hawana uwezo wa kuyatumia hayo katika uhalisia.
Ni sawa na mtu ana uwezo wa kuelezea mpira,sijui "alipiga balistic misile moja,ile inaitwa grass cuttered,semi bending spinning ball" chuma kikala waya.
Kwa hii nchi huyu anaweza kuchaguliwa timu ya taifa ijapo anajua nadharia tu.
Nakuomba waziri utoe wito,mambo ya kijinga yaondolewe kwenye elimu kuanzia kindergarten mpaka chuo kikuu.Yapo mengi sana tena yanakwamisha wakati mwingine mtu kumaliza masomo yake.
Hivi hatuwezi kufikiri kabisa jamani ama ni nani aliyeturoga?