Profesa Mkumbo: Uchumi wa Dunia unashuka, ila Uchumi wa Tanzania unapanda


Prof Kitila ni rafiki yangu katika mambo mengi lakini katika hili la "unwarranted social constructionism" huwa tunatofautiana. Hakuna mtu mwenye mamlaka ya kutengeneza ukweli. Ukweli unagunduliwa. Sikubaliani na ugunduzi wake mara nyingi. Hapo tu tunapigana kisogo. Kwa sasa uchumi umesimama. Cash flow hakuna hasa huko vijijini. Simu za kuomba msaada kutoka vijijini kwenda mijini kwa ndugu, jamaa na marafiki zimeongezeka sana!
 
 
Swali la kujiuliza ni je, ukuaji huu unawasaidia wananchi wa kawaida?

Kwa mujibu wa takwimu, zaidi ya Watanzania milioni 25 wanaishi chini ya dola 1.90 kwa siku. Hii inaonyesha kuwa licha ya ukuaji wa uchumi, umaskini bado ni changamoto kubwa.

Pia, mfumuko wa bei umeongezeka hadi asilimia 3.17, na bei za vyakula zimepanda kwa asilimia 5, huku mishahara ya watu ikiwa haijabadilika.

Kwa upande wa ajira, vijana wengi bado wanasota mitaani, na wengi wanafanya kazi zisizo rasmi zenye kipato kidogo.

Ingawa takwimu zinaonyesha uchumi unakua, maisha ya wananchi wa kawaida bado ni magumu. Ni muhimu kuhakikisha ukuaji wa uchumi unaleta manufaa kwa watu wote, na sio kwa wachache tu.
 
Tuna bunge la hovyo mno,sidhani kama kuna nchi ya kutuzidi kwenye hili
 
Acha kabisa!
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜…๐Ÿ˜†๐Ÿคฃ๐Ÿคญ๐Ÿ˜ญ
 
unapotosha wadau madam,
cash flow sasahivi ni kutoka mijini kwenda vijijini, and for your information vijijini kuna hali nzuri zaidi ya kiuchmi kwa sasa kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya Taifa letu.

waziri yuko sahihi, na ameeleza ukweli mtupu kwa uwazi na dunia nzima inaskia.

hata hivyo,
wasiopenda kuskia ukweli itawapashida kidogo hii taarifa ya waziri ๐Ÿ’
 
Nimesoma tu hapo juu sijamsikiliza
How comes? No numbers? Quantitatively! Qualitatively/- Uchumi wa GDP ngapi umekuza ajira kiasi gani, viwanda gani, na imeongeza kipato gani kwa shughuli zipi na mfumuko wa bei??!! Yeye na Ponjoro hakuna tofauti, au Dr. Msukuma.
 

Prof wa kutengeneza sayari ya Tanzania.
 
ni jambo la kutia moyo sana na kufanya waTanzania kua jasiri zaidi katika kujitegemea duniani

๐Ÿ˜„ ๐Ÿคฃ ๐Ÿ˜‚ ๐Ÿ˜† ๐Ÿ˜„ ๐Ÿคฃ ๐Ÿ˜‚ ๐Ÿ˜† ๐Ÿ˜„ ๐Ÿคฃ ๐Ÿ˜‚
 
Kwa hiyo Tanzania sio sehemu ya hiyo dunia ambayo uchumi wake unashuka?

Stupid
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ