Ndagullachrles
Senior Member
- Jun 20, 2023
- 153
- 161
MBUNGE NDAKIDEMI AWAKIMBILIA WAATHIRIKA WA MAFURIKO KATIKA KATA ZA MABOGINI NA ARUSHA CHINI.
Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi ametoa pole kwa Wananchi wa Kata za Mabogini na Arusha Chini ambao nyumba na mazao yao yameathirika kwa mafuriko yaliyotokea katika Kata hizo. Mafuriko na uharibifu huo yaliyotokea tarehe 25.04.2024 yamesababishwa na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha katika mkoa wa Kilimanjaro, hasa maeneo ya milimani.
Ndakidemi alitembelea wahanga hao siku ya tarehe 1 May, 2024 ikiwa ni ziara yake ya kuwapa pole wananchi wa Jimbo la Moshi Vijijini walioathirika na mafuriko.
Wakitoa taarifa fupi kwa nyakati tofauti, Diwani wa Kata ya Mabogini Dr Bibiana Massawe na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mikocheni ndugu Salehe Kulakwa walimthibitishia Mbunge kwamba kwenye maeneo yao hakuna vifo vilivyotokana na mafuriko hayo, bali wananchi wengi wamepoteza makazi yao, na mazao mashambani kusombwa na maji.
Akiongea na wananchi katika maeneo hayo, Mbunge alisema kuwa amefarajika mno kuona kwamba hakuna kifo kilichotokea. Aliwaambia ataendelea kushirikiana nao na viongozi wa Serikali kwenye kukabiliana na changamoto zao.
Akiwapa mkono wa pole, Ndakidemi alitoa msaada wa mahindi tani mbili kwa Wananchi walioathirika ili yasaidie kwenye chakula. Kila Kata ilipewa Tani moja ya mahindi.
Wananchi walimwomba Mbunge awasaidie ili wapate maeneo ya kujenga makazi ambayo hayataathiriwa na Mafuriko. Mbunge alisema atafikisha ombi hilo kwa viongozi wa Serikali.
🇹🇿🇹🇿
Imetolewa na Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Moshi Vijijini
01.05.2024