Profesa Shivji-Maridhiano ya Zanzibar

..ukiona m-Tanganyika anaingilia siasa za Zenj ujue anafanya hivyo with the encouragement ya baadhi ya wa-Zenj.

..vilevile ukiona m-Zenj anaingilia siasa za Tanganyika ujue kuna anafanya hivyo kwa baraka za baadhi ya wa-Tanganyika.

..siasa za Zenj ni kama ndoa[mfano tu] yenye matatizo. wana ndoa wanaweza kutafuta ushauri nje, lakini amani ya kudumu ktk ndoa hiyo itapatikana kwa utashi wa wana ndoa wenyewe.

..lakini mzizi wa haya maingiliano ni MUUNGANO na mifumo ya uchaguzi ya vyama vya siasa.

NB:

..Karume aliwatumia wanamtandao wa Tanganyika kumshinda Dr.Bilali. wanamtandao nao wakamtumia Karume kumshinda Salim Salim 2005.

..ushawishi wa komandoo Salimin Amour kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM toka Zenj ndiyo uliomuwezesha Ben Mkapa kumshinda JK mwaka 1995

..hivi kuna anayeamini kwamba Maalim Seif anaweza kushinda uchaguzi ndani ya CUF bila kupata kura za wanachama wa CUF toka Tanganyika?
 
Hivi visiwa vidogo na vina watu wachache lakini kelele zake si mchezo! Wakifika angalau 5m sijui itakuwaje? Mh, kaazi kweli kweli!
 
Hivi visiwa vidogo na vina watu wachache lakini kelele zake si mchezo! Wakifika angalau 5m sijui itakuwaje? Mh, kaazi kweli kweli!

Babu yako alitamani kuvizamisha lakini kabla havijazama akazama yeye ndani ya ardhi (tomb)...maombi yake hayakutimia maana alichoumba ni batili na laana ya Muumba

Hiki ni kisiwa na nchi ya watu, wenye ustaarabu wao kabla ya ustaarabu wa wazanaki kutoka musoma wa kuchunga mbuzi na hata wa Tanganyika wote...kila anayedhulumiwa lazima atadai haki zake natural human behavior

Wale wanaodai wao hawaoni kama kelele ila madai, wanaodhulumu hawapendi madai wanaziita kelele...

Wanzanzibar embu pazeni sauti zenu kwa pamoja hadi kelele (madai) yenu yapasue masikio yao washindwe mpate haki zenu za kuishi kwa ustaarabu wenu wa miaka nenda rudi..it is time.
 


kauli yako inaashiria imani yako kuwa wabara tunafaidika na Muungano ule. Hapana, in fact Muungano ule unawasadia sana wazenj kwa vile wanapata madaraka huku bara wakati wabara hawawezi kupata madaraka huko Zanzibar.

Kwa vile wazanzibar mnaonyesha kuwa hamuutaki kabisa muungano ule, hilo ni jambo zuri sana. Mnachotakiwa kuanza kufanya ni kukana kabisa yale Mapinduzi ya mwaka 1964 kuwa yalikuwa haramu, na kurudisha serikali halali iliyokuwapo ikiongozwa na Shamte kwa vile ndiyo iliyokuwa imechaguliwa kwa mujibu wa Katiba. Baada ya mapinduzi, katiba ilifutwa na watu wote waliochukua uongozi wa nchi hawakuwa wamechaguliwa na raia.

Ila kama mtendelea kukubali kuwa mapinduzi yalikuwa ni halali, basi makubaliano yaliyofanywa na viongozi wa mapinduzi yale yalikuwa nayo ni halali, ndiyo maana muungano ulioridhiwa na Karume utabaki ni halali, kwa sababu Karume ndiye aliyekuwa kiongozi wa serikali ile ya mapinduzi.
 
Baada ya kusoma article ya Shivji, sidhani kama kweli anakubaliana na mependekezo yaliyotolewa na Hamad kuhusu kumuongezea muda karume ili eti aondoe "siasa za chuki" Zanzibar. Alichosema na kuwa jambo hilo linawezekana lakini kwanza lazima Baraza la wawakilishi liweke sheria mpya maalum alioita "constituent act" ambayo ina nguvu sawa na Katiba.

Jambo ambalo Issa hajajibu ni kuhusu position ya Bunge la Jamhuri ya Muungano katika swala hili; kwani uchaguzi wa Rais wa Zanzibar unatawaliwa pia na Katiba ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo ni lazima vifungu vya Katiba hiyo pia vifanyiwe marekebisho.
 
Mwana kijiji< Hebu unapoiandika usiogope kuandika vilivyo. Mwenye kuandika historia ya zanzibar ni nani?. Kama ni maalim Seif basi mtaje watu wamjue sio wakati wa kuficha. Historia ya zanzibar haikuanza 1964 wala sio ile alioilazimisha Mapuri isomeshwe shule na wala sio hiyo unayofikiria wewe kuwa wazanzibari ambao sio waarabu au waasia ilikuwa ni watumwa. Historia yetu tunaijua vilivyo na itaandikwa na wazanzibari wenyewe wala sio wasiokuwa kati yetu maana hawazijui tarekh zenyewe. Wacheni kwanza tuangalie muafaka wetu halafu tutajadili historia. Au nyinyi munapenda zile chuki?.
 
Kichuguu, Kuna mipaka fulani huwa hatuipiti. Kama wazanzibari, sisi tuna katiba yetu na baraza letu pia. Kwa hivo, kuna maamuzi tunao uwezo wakuamua. Masuala ya uraisi wa zanzibari ni masuala ya wazanzibari OK. Masuala ya raisi wa tanzania ni masuala ya watanzania. Kama kulikuwa na tanganyika basi tungelikuwa na masuala ya tanganyika au sio. Kwa hivo, masauala ya zanzibar, hayaihusu serikali ya tanzania. Haya ni yetu mpaka hapo katiba itakapo pigwa kiraka kingine. Kwa leo ilikuwa hamukuliona hili ok. Musitubabaishe kwa porojo za viongozi wenu huko bara.
 
Buchanan: Inaweza kuwa kweli visiwa hivi vina watu kidogo lakini nakufahamisha kuwa uwonevu una mwisho Haiwezekani kila siku ikawa munatupelekesha munavotaka nyinyi tu. Kuna mwenzako anataka kuzungumzia historia. Munajua kama tukizunzia historia, itabidi wengine murudi brundi na rwanda na congo?. Huo mkoa wa pwani wote ni wetu acheni fitina zenu. Sisi tunawaheshimu sana lakini nyinyi munaonyesha madharau sana juu ya wazanzibari.
 
You have identity problem. And I think that is what haunting Zanzibaris.
Try to know to where you belong and come to discuss points instead of writing crap.
Tanzania belongs to you and I also; the way Zanzibar belongs to Tanzania; blame your grandfather Mr. Karume (Senior) instead of the other side, as this Union is here to stay for generations!!
 
Mkoa wa Pwani ni Wenu, justify please; na hayo ndiyo yatatokea! Tangu lini Dar ilikuwa Zanzibar?
 

Ndugu, labda nijitambuliesha mapema kuwa mimi siyo mwanasiasa wala sishabikii upande wowote wa mjadala huu. Kuwe na Muungano au usiwepo hainisumbui kabisa kwa vile sioni tofuti yoyote katika maisha yangu.

Baada ya kujitambulisha hivyo sasa turudi kwenye mjadala, ni kuwa baada ya kusoma kwa makini katiba ya jamhuri ya Muungano Sura ya 4 sehemu ya kwanza nimebaini kuwa Raisi wa Zanzibar anapata madaraka yale siyo tu kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar bali pia kwa mujibu Katiba ya jamhuri ya Muungano. Ndiyo maana nikasema kuwa iwapo sheria aliyopendekeza Issa itatekelezwa na Baraza la wawakilishi, basi lazima Bunge la Jamuhuri ya muungano nalo lichukue hatua fulani ili kuhalalisha uamuzi huo.

Kama Taifa tutadumu tu kama tutajenga utamaduni wa kuheshimu katiba na sheria zetu, siyo tu kwa vile mtu fulani ana madaraka basi sheria na katiba havimhusu.
 

..Wanao wagawa Wazenj ni wale wanaojifanya wanaijuwa sana Zenj kuliko wao wenyewe, wale wanao waimbia wimbo wa HISTORIA HISTORIA HISTORIA, historia walizo zibuni wao kwa malengo yao. Nchi zote zimetawaliwa nahivyo wanahistoria zao, zile nzuri hukumbukwa na kuendelezwa, zile chafu hutupwa na kusahauliwa ili watu waishi pamoja. Hata Wazanzibar wanao uwezo wa kuzisahau historia chafu. waacheni wazanzibar wamalize matatizo yao MSIWACHANGANYEEEEH
 
Crap! siwezi kudiscuss utumbo..zanzibar waachieni wenyewe mnataka nini?

Always crying crying! alianza babu yenu nyerere leo nanyi mnaendelea kulia lia zenj..mnang'ang'ania nini? waacheni na nchi yao

Mmeshindwa kuwasaidia watu Kigoma, Tabora, Ruvuma maji ya kunywa mnajisikia raha na kujidai siasa za zanzibar na kujidai mnawapenda wazenj shame on you
 

Pole!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…