Profesa Tibaijuka anaweza kushtakiwa kwa money laundering?

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
20,925
Reaction score
51,688
Je,Prof Anna Tibaijuka anaweza kushtakiwa kwa money laundering?wataalam wa sheria karibuni
 
Pamoja na Mkombozi Na Stanbic, Sheria hairuhusu cash ya bil. 75
 
Money Laundering ni utakatishaji/ usafishaji wa fedha chafu. Kwa mfano, hizo 1.6B zikitumika kujenga mgahawa na Ikiwa watathibitisha kuwa ile transfer ya kupitia shule ilikuwa ni njia tu ya kupoteza lengo au kuhalalisha chanzo basi hapo anaweza kubanwa na case ya ML.
 
Kwa kumshitaki Prof. ni kumuonea kwani hizo pesa zinazodaiwa kuchukuliwa na Mheshimiwa sio kwa manufaa yake bali ni kuinufaisha shule kwa ajili ya kuwasaidia watoto wanaosoma katika shule hizo na wanauwezo wa chini, pia sio hao tu hata wengine anawalipia wapo vyuo vikuu .Ningewaomba wananchi msiseme maneno tu bila kuwa na uhakika wa maneno mnayosema.
 
inasemekana baada ya siku mbili alizitoa zote na kuziweka kwenye personal account yake hapo ndio msingi wa hoja yangu
 
Sasa DuppyConqueror kama ni hivyo mbona issue inakuwa tata zaidi.

Na serikali pia imeagiza hao wanufaika wa mgao(rushwa/takrima???) walipe kodi ya mapato, so serikali nayo inatakatisha hizo pesa?
 
Last edited by a moderator:
Wanasiasa inabidi waende CRASH PROGRAMME ya sharia pale Mwigulu aliposema eti wana-ESCROW walipe kodi ndo aliharibu kabisa
 
atashitakiwa kwa money laundering kama hiyo 1.6b itathibitika kuwa lilikuwa ni zao la kilalifu, yaani ilipatikana kutoka kwenye jambo la kihalifu na yeye wakati anaipokea alijua imetokea kwenye uhalifu...kupokea tu/possession as long as you have knowledge hata kama haujaitaktisha bado...inatosha, mfano wizi, madawa,rushwa,n.k (yameorodheshwa kwenye sheria kama predicate offences). lakini kama hiyo hela aliipata toka kwa rafiki yake rugemalila kama zawadi tu, ina maana hiyo hela sio zao la uhalifu(proceed of crime) hivyo hawezi kushitakiwa kwa money laundering. money laundering ni utakatishaji wa fedha iliyopatikana kiuhalifu ili iingie kwenye mfumo msafi ionekane nayo ni safi....yaani unaficha ule uchafu ili pesa ionekana safi kwa kuitakatishia kwenye vitu visafi ili pesa chafu nayo ijifiche kwenye usafi ionekane kama ilitokana na usafi kumbe sio.

kwa hapa maza prof tumeshamkosa kwasababu hela hiyo alipewa zawadi kwaajili ya shule na rugemalila na rugemalila aliipata kihalali na alilipa kodi. labda kama hela hiyo angekuwa ameipata toka kwa mhindi aliyekuwa amekwepa kodi na hapohapo lazima iwepo knowledge ya maza prof kuwa hela hiyo ni proceed of crime. wabunge wanahitaji shule, tatizo huwa wanajifanya wanajua kumbe mambulula.
 
Hapa sana hata mmnaona ni kosa la maadili ndio litamuhukumu ikithibitika alipewa kwa nia ya kumsaidia huyo mtoaji ili apate favour yeyote serikalini kupitia maza prof.
 
inasemmekana tu hakuna aliyeona na kama zilitolewa bado zinatumika kunufaisha shule na watoto wengine wenyeuwezo mzuri kimasomo lakin hawana uwezo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…