ukwaju_wa_ kitambo
Senior Member
- Sep 15, 2024
- 150
- 173
VERSE 1. ( PROFESOR JAY)
"Usiniache mupweke utafanya watu wanicheke/ ni wewe pekee uliyefanya mi ni deke/ kuvunja mpenzi letu utafanya mi niteseke/ nisieleweke mwenzio mi nizeeke/ ni upumbavu wangu uliofanya penzi limegeke/ na hila za vicheche kufanya nafsi ilogeke/ ni shetani pekee aliyenifanya ni tetemeke/ nikajifanya mbwa kila dakika ni bweke/ usisononeke maisha ni seke seke / ndani ya moyo wangu mkuki usi uchomeke/ penzi lako la dhati lilifanya nafsi uiteke / nika geuka punda shukurani zangu mateke/ sihitaji wakili ili hukumu isomeke/ nisamehe ili makosa yasiongezeke/ kwako napiga goti ili nadhiri Niweke/ penzi ni kama safina pande gani tuipeleke/ usitetemeke bibie usiboreke / rundisha moyo nyuma mapenzi yaongezeke/ sijui nifanye nini ili msamaha uombeke/ nieleweke na mwishoe tu meremete /...
Ukwaju wa kitambo
0767 542 202