Professor Jay & Chid Benz (msilie)

Professor Jay & Chid Benz (msilie)

ukwaju_wa_ kitambo

Senior Member
Joined
Sep 15, 2024
Posts
150
Reaction score
173
1726526160377.jpg
PROFESOR JAY FT CHID BENZ - MSILIE. ( PRODUCER LAMAR) 41 records..


Verse .. 1.

Yeah! Na muomba Mungu ili tuweze kuyakabili/ yanayojili mengi wahenga waliyatabili/ ona nyumba za ibanda leo zimengeuka biashara/ unapata neno la Mungu baadae tiba mbadala/ unafanya usichopenda Wana hubiri wasicho tenda/ maisha yanabadilika midhili ya mfumo wa kalenda/ Kila mmoja anaota neema na utakaso hawakumbuki mema walio nena kwenye viapo/ najua hakuna marefu yasiokuwa na ncha/ jongoo anapowika tambua ndio kunakucha/ thamani ya mtanzania sio madeni na ukabuku/ tumelalia utajiri ili tungoje rudhuku/ nipe Ubora wa Elimu na sio wengi wa Takwimu/ mbona mna nunua siraha badala ya kuwalipa walimu/ maisha Bora Kwa wote ndicho nachopingania/ hiki kivuli chetu hatuwezi kukikimbia..

Chorus..

"Msilie" kwenye Taabu pinga moyo konde/ "msilie" jipaze juu sauti ya mnyonge/ "msilie" tupinge koti tuombe maisha ni mchanganyiko wa milima na mabonde × 2

Verse 2..

" Msilie" watu wangu wa kweli mliopo jela/ wote tunaelewa maisha huko mpela mpela/ wengi kweli mlikosa wengine mmesingiziwa/ Salama na Afya zenu ndio kitu cha kuzingatiwa/ haja kubwa kwenye mtondoo/ wengi mnapata "tb" wengi wanakata roho sababu ya h.i.v/ mateso Kwa wafungwa yamepitishwa kama sera/ sijui niite utumwa au uhuru wa bendera/ wazawa tunaunga tela kama tumeunga kinyesi/ unaulizwa kwanza hela pindi unapokuwa na kesi/ Rushwa imeshika hatamu karibu itakuwa halali/ tajiri anatoa hongo na polisi ndie dalali/
Machinga waliofukuzwa wengi wamepoteza ajira/ wengi wamejawa na hasira wengi wameamsha dhamila/ msilie Amani yenu ndio itawaponya/ na mikikata tamaa mlichonacho mtapokonywa..

Chorus..

Msilie" kwenye Taabu pinga moyo konde/ "msilie" jipaze juu sauti ya mnyonge/ "msilie" tupinge koti tuombe maisha ni mchanganyiko wa milima na mabonde × 2

Verse..3.

Vyanzo vyetu vya maji kila siku vinakauka/ msitu inakatwa inaanguka/ Taifa linanuka Rushwa/ madini yanachibwa nje yanavushwa/ mabilioni ya B.o.t yamenyenyuka/ Na Tupo makini kusitunza na kuenzi mali za Asili/ Mbunga zetu zimetekwa na kundi la majagili/ kila tunapoamka hadithi kwetu asiishi/ majambazi Wana siraha zaidi ya polisi/ msilie wajawazito mnaoteseka hospitali/ omba omba mnaoshinda juani kusaka ugali/ hayo yote ni maisha na siku zinahesabika/ shida zimeubwa kwetu na Duniani ni uwanja wa vita..

Chorus..

"Msilie" kwenye Taabu pinga moyo konde/
"msilie" jipaze juu sauti ya mnyonge/ "msilie" tupinge koti tuombe maisha ni mchanganyiko wa milima na mabonde × 2

Hii hii ilitoka mwaka 2007 katika studio za 41 records producers akiwa "lamar" project za mwanzo kabisa professor jay kufanya na producer lamar baada ya kufanya Kazi nyingi hapo nyuma na producer p funk majani kutoka Bongo records ..
Follow page yetu Facebook ya UKWAJU WA KITAMBO

Mawasiliano 0767542202
 
Back
Top Bottom