Professor Jay kuja na hip hop singeli, afafanua kwanini amerekodia video yake ‘uwanja wa fisi’,

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906

Staa wa Hip Hop na Mbunge wa Mikumi, Joseph ‘Professor jay’ Haule, wiki hii anatarajia kuachia wimbo wake mpya aliyochanganya mahadhi ya Hip Hop na Singeli aliyomshirikisha Shollo Mwamba.

Akizungumza na ripota wa Timesfm.co.tz, Jay, amesema wimbo huo unaitwa kazi kazi ukiwa na lengo la kuwahamasisha waliokata tamaa kuamini kuwa kila kitu kinawezekana ukifanya kazi kwa bidii.

“Ndiyo maana unaitwa kazi kazi na video tumeirekodi kule kule kwenye watu wenye changamoto na waliokata tamaa kuwahamasisha zaidi, uwanja wa fisi, kama kipande kinahitaji m*laya tumewatumia wahuisika kweli.

“Nmechanganya na Singeli ili kuipa sura mpya Singeli, watu wa singeli wanaonekanaga wahuni, muziki wa kihuni sasa nataka tuwasaidie kwa sababu ni aina yetu ya muziki wa hapa nyumbani, tumewatumia wakabaji kweli kwenye video na watu walifurahi kumuona Mbunge ameingia maeneo yao” Amesema.

Wimbo huo umetayarishwa na Mensen Selekta, Video imeongozwa na Kwetu Studio na ‘kazi kazi’ itaachiwa rasmi Ijumaa wiki hii.















 
Kuna huyo jamaa kwenye picha kavaa jezi ya Arsenal,yaani sijui mkikutana nae kwenye kichochoro kama atakuacha salama...Hatari sana!!Huyo ofisi yake ni bisbisi(?) na wembe!!
Hahaha! jamaa anaangalia kwa uchu sana, anatamani kutokee miugiza hapa kuwa na kiza cha gafla atembee na kichwa cha mtu hapo
 
Kuna huyo jamaa kwenye picha kavaa jezi ya Arsenal,yaani sijui mkikutana nae kwenye kichochoro kama atakuacha salama...Hatari sana!!Huyo ofisi yake ni bisbisi(?) na wembe!!
Umeambiwa wamechukuliwa wahusika wa u kweli sasa hapo tegemea roba ya mbao sio ajabu ila jamaa mkavu flan hivi kauzu kauzu anaonekana mbandidu kimtindo.
 
Dah hili dude nimekuwa nikiliskiliza siku nzima leo....Bonge la message na jay ameflow utamu sana na biti la singeli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…