Upekuzi101
JF-Expert Member
- Aug 28, 2020
- 221
- 542
Ni kweli Tanzania tunahaja ya kujitanabaisha kimuziki na kuwafanya watu wajue utambulisho wa muziki wa Tanzania. Kuna mirindimo inapaswa kuwa utambulisho wa muziki wetu ila kiukweli hapa kwa singeli haujawaza sawa sawa. Mziki inapaswa kutambuliwa ni muziki wenye mirindimo na midundo yenye staha, uchezaji wa heshima na maadili yenye kusisitiza nidhamu pia. Hivi vyote havipatikani kwenye muziki wa singeli, muziki wa singeli nafikiri ulipaswa kuwa muziki au nyimbo za unyagoni labda ila kwa midundo, mirindimo, uchezaji na hata utunzi wa Hizi nyimbo umekuja kitofauti ukiambana na kucheza uchi, kuimba matusi, mbele ya vijana wazee na watoto, nadhani huu muziki hauwezi kuwa utambulisho wa Tanzania. Kazi ya sanaa ikiwepo muziki, una kazi ya kuburudisha, kufundisha na kuonya jambo ila singeli inapoteza au inashindwa kukamilisha Hizi sifa kwa usahihi kwaiyo bado ni changamoto kuupa hadhi kubwa namna hiyo. Muziki. Muziki unaoimbwa sasa vijana wanauita bongo fleva, huu muziki una mchanganyiko wa midundo mbalimbali ya kiafrika, flow mbali zenye mchanganyiko wa vibwagizo kutoka kwenye makabila tofauti ya wananchi wa Tanzania na hata nchi nyingine kutoka Africa. Mheshimiwa Kabudi Bongo fleva ndo muziki wa Tanzania, tafuta namna sahihi ya kuweka mawazo sawa, kutana na wadau wa sanaa wakusaidie mawazo ufanye vyema ila hapa kwenye singeli "you didn't do your homework well"