Proffesor Jay amtembelea Diamond ofisini kwake, amfagilia kwa uwekezaji alioufanya na mawazo mapana

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506



Mbunge wa Mikumi ambaye ni msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop, Joseph Haule ‘Professor Jay’ Jumatatu hii alitembelea ofisi za WCB na kujionea uwekezaji uliofanywa na rais wa label hiyo Diamond Platunmz.

Akiongea na Bongo5 Jumanne hii, Professor Jay amemsifia Diamond kwa uwekezaji aliyoufanya.

“Kikubwa kwanza nitumie nafasi hii kumpongeza Diamond kwa kuwa na mawazo mapana zaidi kwa sababu kiukweli kwa wasanii wengi wa Tanzania na Waafrika wengi tunaweza tukawa na kipaji lakini mazingira yetu ya kazi yanakuwa magumu,” alisema Professor.

Aliongeza, “Kwa mfano pale kwa Daimond jana nimeenda nimekuta kuna studio hapo hapo, pamoja na kurecord lakini pia anachumba ambacho amekitengeneza cha kutengeneza photoshoot. Lakini pia ana sehemu ya kufanya editing ya kazi zake na ana watu special ambao amewaajiri kwa ajili ya kazi hizo, hii ni hatua kubwa sana kwa msanii,”.

 
Nasikia baada ya ujio chid benz wasafi..pale studio walitoa lile sanamu la kichwa cha mtu wameweka bangi
 
Safi sana, bila shaka angependa kumtembelea mzee wa Ndovu lakini tatizo atamkuta wapi maana jamaa hana ofisi.

Si vema mbunge kwenda Saigoni kwa ajili ya mazungumzo na babu K.
 
Prof na wewe ile studio yako iliishia wapi?
YNWA
 
Akina Proff haya ma aidia hawakuwa nayo nadhani dogo amepata exposure ya kutosha ndio maana anazidi kutanuka kibiashara...
 
Diamond inaelekea anapenda sana kuvaa mabazee
 
Hatua aliyofikia DIAMOND ingekuwa ndio ya yule mwingine humu ndani kungekuwa na thread 50+.
 
Kati ya Maprofesa wote Tanzania Profesa Pekee ninaye mkubari ni Profesa Jay.
 
Hatua aliyofikia DIAMOND ingekuwa ndio ya yule mwingine humu ndani kungekuwa na thread 50+.
ni nani huyo best hahahahaaaaaaaaaaaaa makubwa kumbe wengine wanapenda masifa sana
 
Du! Prof J umri ndo ivyo tena bye + ubonge huo kwaher
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…