Profile ya Kanumba... kaiandika mwenyewe

Hivi ilikua ni lazima aandike kwa kiingereza? au?


nilipoisoma niliona jamaa anadhani akiandika kidhungu ndio atauzika zaidi, bac angetafuta m2 wa ku edit kama sio kumuandikia upya, kiswa pia ni kizuri jamani.
 


ma bro Maane ha2chekani, ni kwamba wasanii we2 hawapendi ushauri, angependa kushauriwa hata yeye acngeweka hito profile angetafuta hata m2 wa pili wa kusaidiana nae, hii inaonyesha kajiandikia mwenyewe na kubandika moja kwa moja.....ni ushauri tu tunawagea hapa, hawapendi kukosolewa.
 
Hivi mtu ukitumi lugha unayoilelewa vizuri utakufa? nini maana ya wakalimani kama hatutaki kuwatumia? Kanumba tumia wakalimani na bado utakuwa juu tu but ikibidi ingia darasani kidogo tena!
 
tusitafutane wachawi kwenye mambo ya lugha...hii kaandika mwenyewe. literal translation from swahili to english.lol

Mdau mbona unamruka nduguyo?? Just admit kwamba umemsaidia kuandika!!! naona mmevunja (broken) mbaya!!




Just kidding
 
Oh Tanzania!!!! what an embarassing people we are!!! why must some one see the speck in his brother's eyes before removing his own? then what next?is speaking broken English a crime and what penality does such a crime worth? if it is a crime then 99% ot the citizenz are criminals plus the judiciary.
It's even embarassing that the 'Mr. know-alls' are equally comenting in BroKKKKKKKKKKKKKKKKKen English!!!
Cheap brains that are convinced by comedians!!! don't you forget they(comedians) are here to make you laugh and not to believe what they say!!!
If I knew Kanumba before and if I will still be blessed to keep his track, then nothing is going to change my opinion about him, No..nothing, not even a folly commenent from a comic...Shakespear says'some are born great, some achieve greatness yet others have greatness thrust upon them, Kanumba was born great!!!!!!
 

Mkuu wewe pekee ndo embarass person hivi nini kinakushinda kuelewa? watu hawamcheki kanumba coz hajui English tatizo yeye anabisha kua anajua. Mtu muungwana akikosolewa hukubali makosa na kurekebisha ndo kujifunza huko! Ndo maana hata hapa JF kama umekosea unakosolewa then unasema thanks....sasa we ukisoma hiyo profile ya kanumba kweli kulikua na umuhimu wowote wa kuandika kwa Kiingereza? Acha kutetea Ujinga bwana!
 

Duh!!! OMG!!!!!!!!!!!!!!
 
nafikiri inatosha kwa hayo aliyoambiwa. Leteni habari nyingine tuendeleze kijiwe.
 
Nakubaliana nawe Kamilah, ushauri wako ni mzuri nami naungana nawe kuwa: "kanumba ushauri wa bure kwako, kama ni lazima uwasiliane na watu kwa kiingereza tena kikiwa kwenye maandishi, baada ya kuandika kwanini usiwape watu wanaojua vizuri hiyo lugha wakusaidie kukurekebishia kuliko hii aibu unayopata. Inakuwa tabu kama ni lazima kuongea hapo huna ujanja hakuna wa ku-edit but kwenye maandishi hakuna sababu ya wewe kuaibika. Na si lazima kwa kingereza ungeweza kuweka kwa kiswahili na bado ungekuwa star tu mkubwa. Wakina mtitu msaidieni"
Nampenda sana Kanumba, na ametuinua sana Watanzania katika sanaa ya kuigiza. Pia nategemea ataendelea kutuinua Watanzania tuwe na kitu cha kwetu cha kuivunia. Ila namshauri kuchukua mafunzo zaidi ya lugha hiyo... inawezekena. kwani baada ya muda sio mrefu, itampasa kushiriki makongamano ya kimataifa, na itampasa kueleza sela zake na za taifa kwa kiingereza, iwe kwa kuzungumza au kuandika, ili atunukiwe dhamana. Hivyo, jiandae ndugu yangu ili uwe mjumbe bora machoni pako na pa wengine.
Asante,
Amani N.
 
Kanumba jamaa anayo pesa ya kuweza kujisomesha English course, namshauri aache hasira kuchukua watu wanao mkosoa kwa nia nzuri tuu, aingie darasani asome
 
hiyo imetulia sana....... sina mengi. ila wengi wetu wa TZ ni waswahili sana. nadhani naeleweka ninaposema waswahili...locality. jamani tubadilike....tujadili masuala muhimu ...lugha ishu ndogo sana. nivema tukajadili masuala na si watu.....
 
kanumba jitahidi uende shule kuliko kuumbuka namna hii,watu waliona mapungufu uliyonayo katika lugha lakini ukabisha.kanumba ulisema umetengeneza filamu nyingi kwa kizungu,napenda kukueleza kwamba LUGHA YA KIINGEREZA WEWE BADO NENDA KAJINOE UPYA.
 
hi all,
ni vizuri kwamba watu wengi wamechangia hii hoja; bwana kanumba kwa kweli wewe ni nyota hapa tz, na kwingineko. hongera.
lakini ukweli unabaki palepale, kwa kuwa sasa wewe ni star, basi utaitwa sehemu mbalimbali duniani, kama vile ilivyokuwa kwa bb. frankly, mawasiliano yako katika kimombo hayaridhishi; ushahidi mkubwa ni zile "blank faces/expressions" zilizoonekana nyusoni mwa baadhi ya celebrity guests na bb members siku ile ya ufunguzi wakati mzee kanumba ulivyokuwa ukijaribu kuwasiliana nao. wale washikaji celebrity guests walikuwa na uwezo mkubwa wa kujieleza kwa kimombo kuliko wewe ndugu yetu.
kwa kifupi jifunze kimombo, na baada ya hapo tizama tv - vile vipindi serious! - na usome vitabu ili uweze kupanua mawazo yako na kuongeza topic ambazo utaweza kuwa 'conversant' nazo. yule nonhle wa channel o - ambaye alikuwa pia celebrity guest - anaweza kuku-inspire ndugu yangu ili na wewe uweze kujiamini kukaa meza moja na mtu kama yeye ukasema kitu kikaeleweka, kwa kimombo.
narudia tena, soma lugha ndugu yangu, dunia ni pana, imekupenda, na imeanza kukupanulia tabasamu la kukukaribisha. jitayarishe ili na wewe ukitabasamu kuwe na nuru badala ya BLANK FACES! good luck, my brother. go and make us proud.
 
Nilifurahi sana yule young man wa X-PLASTAZ aliyekwenda kwenye Hip Hop awards za BET nafikiri alivyosema kuhusu kiswahili, kasema yeye anaweza kiingereza cha kubabaisha na akijaribu ku rhyme kiingereza watamuotea, lakini lugha ya mama yake ni kiswahili na hiyo ndiyo anachana nayo.hii ilikuwa ni baada ya kuulizwa kwa nini hachani kiingereza.

Simple and clear, admirably so.

I only wish Kikwete na hawa clowns wengine wanaojiaibisha kwa kung'ang'ania kiingereza had the same fortitude.
 
Hata mimi alinifurahisha sana. Hakutaka kulazimisha mambo na akakiri kuwa kiingereza hakipandi. Hakuna kibaya hapo. Kutokujua lugha flani hakumaanishi mtu si mwerevu.
 
Ni vizuri amejeleza ipasavyo lakini katumia lugha isiyo! Ni vizuri kuwa muwazi kama kitu fulani kinakusumbua, hivyo amefanya vizuri kuionyesha jamii kuwa kiingereza kinamsumbua, na si kosa hata kidogo. Taratibu atajua, walatini husema hivi, fabricando fit faber, yaani mfinyanzi hujua kufinyanga kupitia kufanya ufinyanzi, hata Kanumba atajua Kiingereza kupitia kufanya mazoezi ya kuandika na kuongea kiingereza.
 
mi naona mshkaji kajitahidi, mbona hata wakubwa kibao wanajiumauma kwenye lugha mi naona kama vpi hivyohivyo kibongobongo ili mradi tuelewane.
 

kajitahidi japo lugha si sahihi lakini ujumbe unaeleweka na hilo ndiyo la msingi.

hakuna aibu kutojua lugha ya watu kwa uzuri bali ni aibu kwa mbunge kushindwa kujua neno sahihi la kiswahili na badala yake kukopa kwenye kiingereza wakati anahutubia wananchi kule dakawa ambao hawajui kiingereza....bora angeongea kizigua ningemuona wa maana...

mtazamo tu....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…