Profile ya Kanumba... kaiandika mwenyewe

Hivi umeshawahi kwenda China, ukawaona jinsi wasivyo jua "kingreza" na wala haiwashughulishi?? What is Kingreza after all, si ni lugha tu kama lugha zingine ili mradi unamuelewa anamaanisha nini inatosha, labda kama anafungua darasa la "English Literature" ndo iwe ishu kimnyume cha hapa, Go Kanumba Go, tia pamba, songa mbele!
 
tusitafutane wachawi kwenye mambo ya lugha...hii kaandika mwenyewe. literal translation from swahili to english.lol

Mtamliza mwenzenu! Isingekuwa BBA haya yote yasingemkumba
 

Kweli mkuu English is not our motherland language after all
 
Kweli Kanumba hajui kingereza hiyo msikatae,unajua hata katika website yake ameandika Biography kwa kutumia kingereza cha kutafsiri neno moja moja toka kwenye kiswahili kwenda kingereza.

Muundo wa kingereza na kiswahili haufanani na ukiangalia tu utagundua hayo makosa.Masikini hajui kutumia tenses,paragraph,wapi atumie nukta na wapi mkato pamoja na makosa mengi tu.

Msilaumu watu kwa kumkosoa Kanumba.Namshauri Kanumba awape watu wanaojua kingereza warekebishe habari zake kabla ya 'kuziposti' kwenye website yake.Yeye sasa ni kioo cha jamii kwa hivyo watu wanamuangalia kila nachokifanya.

Kwakuwa Kanumba amekuwa kioo cha jamii na mara nyingi anarekodi kwa kutumia kingereza namshauri asome English course pale British council ya miezi mitatu ili aweze kuandika na kuzungumza kingereza fasaha.

Kwa sasa Kanumba hajui kingereza,Huo ndio ukweli halisi.

David
 
Shughuli ipo.nadhani ni changamoto kwa kanumba.He should take it seriously!
 
Steven Charles Kanumba is my name, i was born in a Christian family of 2 girls and i happen to be the last born and the only boy to Mr. & Mrs. Charles Meshark Kanumba.
Mhh nataka tumsaidie kuandika na kurekebisha kwa lugha ya kiswahili:

Wasifu wa Steven Kanumba
Naitwa Steven Charles Kanumba, nilizaliwa tarehe 8 ya mwezi wa kwanza mwaka 1984. Ni mtoto wa mwisho kutoka katika familia ya kikristo ya Bwana na Bibi Charles Meshak Kanumba................................endelea Kanumba

Angalizo mdogo wangu kuna vitu muhimu vya kuweka kwenye wasifu wako usijeweka mwaka wa kutahiriwa kama umetahiriwa, mwaka wa kubalehe, au siku uliyong'oa jino la kwanza n.k.
 
nani kasema english ndo maendeleo au ujanja sana?kwanza ieleweke hii si lugha ya kwanza ya mtanzania je mzungu angeongea kiswahili kibovu tungemdhihaki?hakika tungefurahia! tuacheni ulimbukeni huu wa lugha.
 
Hapa ndipo watanzania tunapopata shida maana umaskini wetu ndo unatuponza,kingereza si lolote si chochote ingewezekana kanumba angeandika kiswahili kabisaa kwenye website yake atakayehitaji tafsiri ya hicho kiswahili awasiliane nae lakini kwa kuutafuta ugali wake inabidi aandike hiyohiyo anayojua ili hata WADHUNGU wasome japo kwa kupindapinda,nenda china au japan uone wala hawahitaji kujua kidhungu,kama unaingia dukani unahitaji nguo unamuonyesha kwa kidole maelewano yanafanyika kwa calculator au pen anakuandikia figure na wewe unamuandikia uliyonayo mpaka mnafikia muafaka unalipa anakupa unachohitaji.POLE KANUMBA
 
Tatizo hapa si Steven Charles Kanumba kutokujua Ki-English, wengi hatujuai, ndio kama walivyosema wengine English is not our mother tongue! Tatizo nilionalo hapa ni kwa nini anang'ang'ania kutumia lugha hiyo! Hao wachina tunaosema hawajui kiingereza kwenye profile zao ambazo zimelenga wasomaji wa kwao hutumia Kichina and it is not a big deal! na zile za kimataifa hutumia wakalimani!. Hata hivyo kwa kuelewa umuhimu wa kiingereza kimataifa, China sasa hivi ndio leading country kwa kupeleka wanafunzi kusoma vyuo vikuu UK, ikifuatiwa na France! ushauri kwa ndugu wane Kanumba hakuna aibu katika kujifunza si uende tu British Council ukasome au kama huwezi/hutaki muone Ras Simba, mbona Joti tulisikia anasoma pale! la kama hutaki kabisa nikukumbushe tu! IF YOU WANT PEOPLE TO UNDERSTAND YOU, THEN TALK THEIR LANGUAGE!
 
Mi naona sawa tu maadam ujumbe umefika. Sisi sio lugha yetu ya kuzaliwa jaribu kuongea na wachina au wakorea usikie!!
 
Mie hata simlaumu, ukizingatia lugha yenyewe ilikuja Tanganyika kwa mashua
 
Mie hata simlaumu, ukizingatia lugha yenyewe ilikuja Tanganyika kwa mashua

Jamani tatizo hapa si yeye kutojua kidhungu, wote humu hatujui vizuri hiyo lugha lakini huwa tunaficha aibu yetu, kama Kanumba angeandika wasifu wake kwa lugha ya taifa nani angesema kitu humu??? Namshauri Kanumba kwa nguvu zote "ACHANA NA KINGEREZA SIO LUGHA YETU NA PIA HUIJUI"
 
baada ya watu kuibamba hii alifungo hiyo website yake faster.....kumkosoa kunamsaidia
 

hapo umenena mkuu.
Mi ninachoshangaa ni umri wake alioutaja hauendani kabisa na sura yake iliyosheheni ''...........''
 
Baada ya kuisoma hiyo Biography nimegundua vitu viwili:
1. Kanumba ni mbinafsi - sikuona haja ya yeye kujikunja na lugha ambayo hajaijua vizuri na kutundika dunia nzima wasome, angeweza kumtafuta rafiki yake anayejua vizuri na akamrekebishia
2. Labda hashauriki - pia inawezekana maana hii ishu ya lugha imemuangusha mara nyingi lakini haelekei kubadilika, mfano kule BBA IV na interviews nyingine anazozifanya
3. Anajiona yupo juu ya kila mtanzania - hili litamuangusha haraka sana, kwa supa staa kudumu kwenye media muda mrefu unatakiwa kuwa na timu ya wataalamu wanaokushauri jinsi ya ku-maintain kukubalika kwako kwa watu, hakumbuki akina Bishanga wako wapi sasa.
 

Duh! Ndio maana alikuwa bubu alipotembelea Big Brother...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…