A
Anonymous
Guest
Kuna programme mpya zinaanzishwa vyuoni hasa vyuo vikuu lakini hazijulikani kwa waajiri. Programme hizi zinaweza kuwa zinampa vigezo mtu aliyechukua hizo programme lakini anashindwa kupata kazi kwa sababu waajiri hawazitambui na akienda kuomba kazi wanamwambia wanahitaji mtu aliyesoma programme fulani.
Kwa mfano: Mtu aliyesoma Bachelor of Arts in Literature anaweza kufanya kazi kama tutor (tutorial assistant) wa masomo ya communication skills lakini soko halimtambui mtu huyu.
Binafsi nimesoma hiyo course na kwasasa nafanya kazi kama part-time wa hilo somo kwenye moja ya chuo cha kati hapa nchini. Changamoto ninayoipata pamoja na wengine waliosoma hii course ni kutotambulika kwenye soko la ajira linapokuja suala la kufundisha communication skills.
Niliwahi kwenda kwenye ofisi za ajira kuwauliza kwanini mfumo wa ajira unatutema wakati tuna vigezo? Niliambiwa kuwa wao wanaweka vigezo walivyopewa na taasis inayotaka kuajiri na sio wao wanaotengeneza vigezo. Je! Ni nani ana jukumu la kuwataarifu waajiri kuwa waliosoma programme fulani wana sifa za kufanya kazi fulani?
Baada ya kutoka utumishi na kupewa hayo majibu nilimtafuta mkufunzi kutoka kwenye department ya Literature (UDSM) na kumueleza hii changamoto akasema sisi (wahitimu wa hii programme) tukaongee na utumishi. Nikamwambia utumishi nimeishaenda na majibu niliyopewa nikampa. Niliona kabisa anapata kigugumizi juu ya hii changamoto japo alisema watalijadiri idarani.
Nimetolea mfano programme niliyosoma lakini zipo programme nyingi sana vyuoni hasa programme mpya ambazo hazitambuliki kwa waajiri hivyo kuwafanya waliosoma hizo programme kuwa na machaguo machache sana kwenye soko la ajira.
Kuna kila haja ya vyuo kuiangalia hii changamoto na kuitafutia ufumbuzi hasa kuzifanya hizi programme zijulikane kwa waajili. Hii inawezekana maana karibia vyuo vyote vina kitengo cha masoko (marketing) ambacho kinabidi kiende mbali zaidi na kuzitangaza programme zinatolewa na chuo kwa waajiri.