Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Ikiwa ni Jumapili, Januari 26, 2025 ni siku ya nne pekee tangu kuzinduliwa kwa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia mnamo tarehe 24 Januari, 2025 mkoani Mtwara, kampeni hiyo imeendelea kuyafikia makundi mbalimbali ya wananchi ili kutoa huduma na elimu ya masuala mbalimbali yanayohitaji msaada wa kisheria.
Miongoni mwa makundi yaliyofikiwa na kampeni hiyo ni pamoja na waumini wa madhehebu mbalimbali ambapo mkoani Mtwara timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria wamefika katika Kanisa la Parokia ya Shangani West kwa ajili ya kutoa huduma na elimu ya msaada wa kisheria.
Akizungumza na waumini hao, Wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Zacharia Mzese amewasihi waumini hao kutumia siku tisa za utekelezaji wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria katika halmashauri zao ili kupata utatuzi wa masuala ya kisheria wanayokabiliana nayo.
Soma pia: Wizara ya Katiba na Sheria yazindua "Mama Samia Legal Aid Campaign" mkoani Iringa. Nchi yetu inaenda wapi?
Nao baadhi ya waumini wa Parokia hiyo wameishukuru Serikali ya Awamu ya sita kwa kuendelea kuhakikisha haki inatendeka kwa wananchi na kuwafikia katika maeneo mbalimbali.
Source: Jambo TV