Mpinzire
JF-Expert Member
- Jan 18, 2013
- 7,503
- 13,463
Kampuni ya ELSEWEDY ELECTRIC leo imefungua kiwanda cha vifaa vya umeme kilichopo Kisarawe, Mgeni rasmi alikuwa Mh Samia Suruhu hasani huku akijinasibu kuwa ataendelea kusafiri ili kuwaleta wawekeza na huku Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akisema kuwa yale ni matunda ya ziara yake kule Misri.
Kwanza tuelewe kampuni ya ELSEWEDY ELECTRIC mara ya kwanza ilifika Tanzania kwaajili ya ujenzi wa Bwawa la Mwal Nyerere kule Rufiji, uwekezaji uliofanywa Kisarawe haukuwa kwasababu ya hisani ya mtu fulani au ziara ya mtu fulani lakini baada ya kampuni hiyo kuona kuna fursa ya kuwekeza kiwanda kwaajili ya kuzalisha vifaa vya umeme hapahapa nchini.
August 24, 2020 Mwakilishi wa Kampuni ya kuzalisha vifaa vya umeme ya Elsewedy Electric ambaye ni Mkurugenzi Mkaazi wa Afrika Mashariki wa Kampuni hiyo injinia Ibrahim Qamar kutoka nchini Misri anayewekeza nchini Tanzania alisema kuimarika kwa Sera, Sheria na mazingira mazuri ya Uwekezaji Nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na amani na utulivu; ndio sababu kubwa zilizomfanya aje kuwekeza nchini.
Tarehe 15 March 2021 Kampuni Ya Elsewedy Iliichagua Tanzania Kama Nchi Bora Kwa Kujenga Kiwanda Cha Kuzalisha Vifaa Vya Umeme Kwenye Ukanda Wa Afrika Mashariki Na Kati
Kwaiyo kuanza kutuaminisha kuwa Safari ya Rais Samia ndiyo imefanikisha uwekezaji kiwanda kile ni uongo ulitukuka.
*******†****************†************†**********†**********
Mwisho kabisa naambatanisha na Hotuba ya Mwalimu Nyerere akiwaambia msijindanganye kuwa mkienda kule kuwafata ndiyo
watakuja.