Projects za Mchungaji Kimaro akiwa KKKT Kijitonyama

Kwa hali hii kama KKKT hawatakaa chini waongee vizuri na Mch Dr Eliona Kimaro, watapoteza big time. Nawashauri wafikirie upya uamuzi wao wa kutaka kumfukuza mchungaji huyu wasije wakalia na kusaga meno hapo baadaye.
 
Hivi kumbe ni project zake binafsi, mimi najua ni project za kanisa na zimejengwa kwa nguvu ya michango ya waumini na ni utaratibu wa makanisa yote ya KKKT hata hapa mbezi beach tuna similar projects na zinafadhiliwa na michango ya washarika
Washarika wanahitaji hamasa ya Mchungaji Kiongozi.
 
Watu wamechukua hili jambo kisiasa sana pasipo kujua kwamba maamuzi ya kanisa ni maamuzi ya taasisi na siyo maamuzi ya mtu mmoja, kanisa lina miongozo yake, taratibu, maadili na miiko na kubwa zaidi viapo

Ifike mahali yuache siasa kwenye mambo yaliyo na uhalisia
 
Kwa hali hii kama KKKT hawatakaa chini waongee vizuri na Mch Dr Eliona Kimaro, watapoteza big time. Nawashauri wafikirie upya uamuzi wao wa kutaka kumfukuza mchungaji huyu wasije wakalia na kusaga meno hapo baadaye.
Watu wabunifu kama Kimaro Ni wa kukaa nao Kwa akili. Vinginevyo unajitengenezea bomu
 
Amefanya mema mengi sana... ila kwa Kijitonyama, mwendo ameumaliza.
Halafu waumini wanakuwa wagumu kweli kuelewa kwamba, mambo yamefikia tamati. Kazi ya Mwenyezi Mungu itaendelea tu, hata kama inapigwa vita.
Akaanze upya anapoweza kuanza. Alimfunika Askofu na wazee wenzake wa kanisa. Anakula minofu yote.
Kama vile Daudi alivyomfunika Sauli...watumishi wema wa Mwenyezi Mungu, toka enzi na enzi, wamekuwa wanabebeshwa mizigo mingi ya lawama na fedheha
 
Miongozo ndio inaumiza Wachungaji?
 
Hivi kumbe ni project zake binafsi, mimi najua ni project za kanisa na zimejengwa kwa nguvu ya michango ya waumini na ni utaratibu wa makanisa yote ya KKKT hata hapa mbezi beach tuna similar projects na zinafadhiliwa na michango ya washarika
Kwani project alizoanzisha mwendazake alizianzisha kwa pesa zake? Mbona anasifika nazo japo hayupo? Watangulizi wake hawakuona umuhimu wa hizo project??
 
Washarika wanahitaji hamasa ya Mchungaji Kiongozi.
Kwani akiondoka Kimaro usharika umekufa? Kabla ya kimaro alikuepo mchungaji mwinginr ambae alihamasisha ujenzi wa kile kitega uchumi,

Kimaro alitoka Kariakoo akaletwa Kijiyonyama ila mpaka sasa Kariakoo bado inaendelea same applies to Kijiyonyama

Waliondoka wakoloni ambao ndio wameleta Uluteri na bado uluteri upo hadi leo itakua huyo Kimaro, hebu acheni siasa
 
Jengo la kitega Uchumi unajua Hali yake Kwa sasa? Ficha ujinga ndugu
 
Kwani project alizoanzisha mwendazake alizianzisha kwa pesa zake? Mbona anasifika nazo japo hayupo? Watangulizi wake hawakuona umuhimu wa hizo project??
Kuna Projects nyingi tu Kimaro alizikuta hapo zimeshaanzishwa, Projects zote za Sharika za KKT ni utaratibu uliowekwa na Dayosisi husika na sio utaratibu wa mchungaji, hata kimaro ameondoka atakuja mchungaji mwingine ataendeleza utaratibu aliokutua
 
Haya basi tumsubirie Dr Anna aendeleze palipobaki. Asante
 
Jengo la kitega Uchumi unajua Hali yake Kwa sasa? Ficha ujinga ndugu
Majengo yote ya vitega uchumi yamedoda, hata la mbezi beach

Nadhani ni worse plan lakini haimaanishi kwamba kanisa limekufa

Miradi yote ya KKKT inajulikana na inapata nguvu kutoka kwa waumini, hata mchungaji akiondoka bado maisha yanaendelea tusitishane
 
Majengo yote yamedoda? Msasani KKKT nako jengo lake limedoda?
 
Kuna Projects nyingi tu Kimaro alizikuta hapo zimeshaanzishwa, Projects zote za Sharika za KKT ni utaratibu uliowekwa na Dayosisi husika na sio utaratibu wa mchungaji, hata kimaro ameondoka atakuja mchungaji mwingine ataendeleza utaratibu aliokutua
Sasa kama ni utaratibu uliowekwa na Dayosisi hizi re-shuffle za wachungaji zina maana gani?
 
Kwa hali hii kama KKKT hawatakaa chini waongee vizuri na Mch Dr Eliona Kimaro, watapoteza big time. Nawashauri wafikirie upya uamuzi wao wa kutaka kumfukuza mchungaji huyu wasije wakalia na kusaga meno hapo baadaye.
Aaa wapi!

Kazi ya Mungu itaendelea bila hata ya Kimaro. Hawa ni watumishi tu na msiwakuze sana kiasi cha kuwapa utukufu. Mungu Atainua wengine na pengine bora zaidi. Tufike mahali tuache kuabudu watu na waabudiwa hawa nao watambue kuwa wanaweza kuondolewa na hata kufa wakati wo wote lakini kazi ya Mungu itaendelea!

Kimaro ajirekebishe. Ajishushe. Aombe msamaha na aendelee na wito wake - Kijitonyama au kwingineko. Na Mungu Atazidi kumtumia.
 
Sawa ndugu abdala, asalam alekumu ndugu yangu
KKKT mnajimaliza. Tunawaonea wivu Kwa dhahabu mnayoichezea. Unajua Kwa nn hakuna projects za maana Kwenye misikiti mingi? Governance!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…