Proof: Binadamu alitengenezwa na Aliens

Huwezi kuthibitisha mpaka unakufa

Na mimi sipo hapa kutafuta uthibitisho, sina muda huo na nafahamu huwezi, hata ukimfufua yule kiongozi wenu aliwarithisha amani yenu hawezi

Ni heri useme hujui hii kidogo itasaidia kuliko kuongea kana kwamba una uhakika wakati ni jambo la kiimani..!

Ila kwa kufikiri kwa njia ya kuwaonea huruma watu wa dini tunaweza sema mungu yawezekana alikuwepo ila Kafa, au kidogo yawezekana kasafiri maeneo ya mbali na hajishughulishi na mambo ya wanadamu_hapo kidogo inakuwa safi
 
Nacheka sana. Muwe mmejipanga mkiwa mnataka kujadiliana mambo ya kielimu, siyo mnaleta utoto na kazi hamuiwezi.

Kazi yangu nimemaliza.

Ahsante sana.
 
Nacheka sana. Muwe mmejipanga mkiwa mnataka kujadiliana mambo ya kielimu, siyo mnaleta utoto na kazi hamuiwezi.

Kazi yangu nimemaliza.

Ahsante sana.
Kazi gani uliyomaliza.!? Iyo ya kushindwa kuthibitisha mungu yupo au ipi.?
 
Kwanini unasema hivyo kwamba Mungu yawezekana alikuwepo na kwanini isiwe yawezekana yupo?
 
Kwanini unasema hivyo kwamba Mungu yawezekana alikuwepo na kwanini isiwe yawezekana yupo?
Hadhari: wazo hilo nimelitoa baada ya kuwaonea huruma watu wa dini

Na nimetoa mapendekezo mawili kama umenisoma, kwamba yawezekana alikuwepo ila kafa au yupo ila kasafiri sehemu za mbali na hajishughulishi na wanadamu

Hii ni dhana isiyo na uhalisia ni vile tu nionavyo mimi kwa mtazamo wangu na haibadili uhalisia

Labda tujaribu kujadiri hizo dhana na si vingine
 
Halafu hapo hapo anashindwa kuthibitisha, sasa kujadiliana na mtu kama huyu ni kupoteza muda, na kwanini wanaishi kwa dhana, na kuzifanya dhana zao ndiyo ziwe "Facts". ?
Wenzako wanasali insha huko nawasikia, nenda kasali kwanza labda ukitoka huko tutaelewana
 
Ndio kuna kitu kinajiumba chenyewe kama vile Mungu,na mifumo ya kifedha(hii ime evolve haina mwanzilishi)
Kwa upande wa hapana, hakuna kinachoweza kujiumba,tunarudi kuwa kila kitu kina mwanzo, na kama ni hivyo basi inakuwa ngumu kusema Mungu hana Mwanzo/Kajiumba/Katokea
Swali la pili sijalielewa.
Hii njia unayotumia ni ndefu ungenisaidia mkuu.Huenda ni wakati wangu wa kujua kwa kuwa nimekutana na mtu mwenye UHAKIKA.
Tatizo unatu "dogosha" na kutushambulia zaidi kuliko kutupa hiyo elimu.
Au naweza kusema hautaki tujue ila tuogope tu na kumfata Mungu blindly,kitu ambacho nadhani hata yeye huenda asikipende
 
Sasa Jurjani unataka nichague upande au nikae kimya😃😃.Mimi nimeongelea possibility ya kuwepo au kutokuwepo kwa Mungu na nikaonyesha kuwa jibu la dhati kabisa ni sijui.Sasa utachaguaje upande katika jambo usilolijua, hiyo ni kwenda kiupofu upofu.
 
Nimekuelewa na ndio swali langu nilitaka kujua msingi wa hizo dhana?
 
Ila mkuu hauoni kuwa lazima kiwepo kisicho na mwanzo ili ndio kiwe chanzo cha kupatikana mwanzo wa vitu?
 
Ndio kuna kitu kinajiumba chenyewe kama vile Mungu,na mifumo ya kifedha(hii ime evolve haina mwanzilishi)
Thibitisha hili.
Kwa upande wa hapana, hakuna kinachoweza kujiumba,tunarudi kuwa kila kitu kina mwanzo, na kama ni hivyo basi inakuwa ngumu kusema Mungu hana Mwanzo/Kajiumba/Katokea
Siyo kweli kwamba kila kitu kina mwanzo.
Mwanzo/Kajiumba/Katokea
Nani amekwambia mwanzo ndiyo kujiumba au ndiyo katokea, unaposema ametokea inabidi utuambie hapo kabla alikuwa wapi ?
Swali la pili sijalielewa.
Swali la pili, namaanisha "create a thing from nothing" (utaniweka sawa hapo kwenye kiingereza).
Hii njia unayotumia ni ndefu ungenisaidia mkuu.Huenda ni wakati wangu wa kujua kwa kuwa nimekutana na mtu mwenye UHAKIKA.
Mara nyingi njia ndefu huwa ina uhakika na yenye kudumu, na elimu inapatikana kwa muda mrefu siyo ghafla tu, kwahiyo kuwa nasubira.
Tatizo unatu "dogosha" na kutushambulia zaidi kuliko kutupa hiyo elimu
Lazima niwadogoshe sababu huwa mnajiona nyinyi ndiyo mnafikiria sana kuliko wengine, jambo ambalo halikuwahi kuwa kweli,hakuna wanao fikiria mambo kwa undani na uhalisia kama watu wa imani ya dini, tena ile dini ya mitume na manabii wote.
Au naweza kusema hautaki tujue ila tuogope tu na kumfata Mungu blindly,kitu ambacho nadhani hata yeye huenda asikipende
Kuhoji ni jambo jema sana ila kuhoji ujinga ni kosa kubwa sana.

Ukitaka kujifunza lazima uwe tayari kwa kujifunza siyo useme tu unataka kujifunza. Swali, je uko tayari kujifunza ?
 
Siyo kila jambo lina hali wezekano, kuna mambo hayana kinyume chake, hasa chanzo na muumbaji, ndiyo maana kulazimisha "possibility" iwepo sehemu ambayo haipo ni kupoteza muda kujidanganya tu, achilia mbali hizo "possibility" unashindwa kuziwekea ushahidi, ni ishara mbaya sana kwa mtu aliyepewa akili.
 
Nimekuelewa na ndio swali langu nilitaka kujua msingi wa hizo dhana?
Zinawezekana vipi kuwa msingi.!?

Msingi wa kitu hujengwa na uhakiki wa jambo ikiwa na maana uthibitisho hauwezi kukwepeka hapo ndio unaweza kusema jambo hili ni lamsingi au lina msingi maana linamatokeo ya uhakika

Na hiyo ni hatua ya mwanzo kwenye fani ya kisayansi ambapo dhana,uchunguzi,uhakiki na matokeo havikwepeki

Mimi kusema mungu kafa ni dhana iliyo kwenye hatua tuseme ya pili ya uchunguzi ila sijafikia ya tatu ambayo ni uhakiki

Kuniuliza msingi wa dhana inakuwa kauli yako bado haijakaa sawa ikiwa kitu chenye bado kinachunguzika

Dhana ni kutunga mawazo katika mtoririko wa kimantiki tunaweza sema kuunga doti kisha kuyafanyia kazi mawazo kwa matokeo

Lakini ni vibaya kuyapa uhalisia kama haujahakiki na wengi ndipo wanapokwama
 
Kwahiyo dhana yako kwamba pengine Mungu itakuwa alikufa au amesafiri imetokana na hatua ya uchunguzi ila hujafikia hatua ya uhakika?
 
Kwahiyo dhana yako kwamba pengine Mungu itakuwa alikufa au amesafiri imetokana na hatua ya uchunguzi ila hujafikia hatua ya uhakika?
Sina uhakika ndio maana nadhani kafa au kasafiri ningekuwa na uhakika ningetoa tamko moja tu

Ni dhana tu kama ile inayosema yupo huku Haina uhakiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…