Proof: Binadamu alitengenezwa na Aliens

Sina uhakika ndio maana nadhani kafa au kasafiri ningekuwa na uhakika ningetoa tamko moja tu

Ni dhana tu kama ile inayosema yupo huku Haina uhakiki
Ishu sio kuwa na uhakika maana hali ya kuwa na uhakika inaweza kupatikana hata katika jambo ambalo si la kweli katika uhalisia wake,navyojua mie kuwa na uhakika ni kinyume cha kutokuwa na mashaka. Mfano mtu akikudanganya jambo na akakupa hadi ushahidi wa uongo na mwishowe ukakubali,ni wazi utakuwa na uhakika juu ya hilo jambo lakini kumbe kiuhalisia unachokijua si kweli umedanganywa.(kwa mtazamo wangu,naweza kusahihishwa)

Kwa hiyo swali langu nilitaka kujua sababu iliyopelekea kujenga dhana kama hiyo ni kipi kilichokufanya ujenge dhana za aina hiyo?
 
Dhana hizo ninazo toka kitambo ila mtoa mada kazidi kuwekea nyama

Kwamba kupitia sayansi ya baiolojia wameweza kutambua kuwa kuna asilimia kubwa ya dna zetu wanadamu hazijishughulishi ipasavyo kwenye mchakato wa utengenezaji wa protin mpya na wakaziita junk dna kwa muono wao

Ikiwapelekea kuhisi labda zilipandikizwa na kitu fulani kutoka maeneo ya mbali ya ulimwengu

Na kuna dhana nyengine zikijaribu kueleza utata wa uwezekano wa uwepo wa maji katika dunia yetu kana kwamba yalipandikizwa kutoka maeneo ya mbali maana si rahisi kwa eneo ambalo ipo kwenye mfumo wetu wa jua kuwa na kimiminika kama maji

Yapo mengi yanayoashiria utendaji wenye ufamu mkubwa kuwahi kuwepo ila bado tunakusanya taarifa hatujafikia hitimisho
 
Kwahiyo ulichoeleza hapa ndiyo kilichofanya ujenge dhana ya kwamba yawezekana huyo Mungu kuwa kafa?
 


Strong points
 
Kwahiyo ulichoeleza hapa ndiyo kilichofanya ujenge dhana ya kwamba ya kuwa yawezekana huyo Mungu kuwa kafa?
Sio hayo tu na mengine mengi

Ila kwa yale niliyoeleza hapo juu ile ya kusafiri na kutupiga chabo kwa mbali inawiana kidogo, kuliko iyo ya kufa mpaka siku nikipata uhakiki wa kaburi lake itafaa kuitumia

Halafu kingine maisha yanaelekea kutokuwa na maana yeyote ile ni masumbuko yenye kelele nyingi na mwisho mbovu, kupitia hilo yawezekana kweli kajificha ili kukwepa lawama nyingi, na mimi simlaumu kwa hilo

Dhana haziishi ila kama tunataka kwenda sambamba na mtoa mada ile dhana moja aliyojaribu kuilezea juu ya hao wageni kupata athari za radiation na kutaka kuhifadhi gene trait zao kwa matumizi ya baadae kidogo inaleta maana japo haina uhakiki, kuliko za hao wanaoitwa wa dini
 
Bado nashindwa kukupata vizuri,suala la kuhusu Mungu ni pana zaidi haliishii kwenye uumbaji au utengenezaji wa binaadamu tu. Sasa hizi dhana zako nashindwa kuelewa umezijengea kwa Mungu wa aina gani au umekusudia nini unaposema Mungu?
 
Bado nashindwa kukupata vizuri,suala la kuhusu Mungu ni pana zaidi haliishii kwenye uumbaji au utengenezaji wa binaadamu tu. Sasa hizi dhana zako nashindwa kuelewa umezijengea kwa Mungu wa aina gani au umekusudia nini unaposema Mungu?

Niambie kwanza ni kwanini unahisi suala la mungu ni pana sana kiasi kwamba halipaswi kuishia kwa uwepo wa wanadamu..?

Nini hasa kinachokupekea kuona binadamu hatoshi kwenye kuangazia habari za mungu mpaka iwepo hiyo ziada.?

Labda ukipata kulijua hilo utaelewa kile kinachopelea mimi kuwa na mtazamo huo
 
Sina maana hiyo uliyoelewa wewe,nachokusudia ni kwamba Mungu anahusishwa na mambo mengi hivyo habari za kuhusu Mungu ni pana si suala la aliyeumba au kutengeneza binaadamu tu. Sikuwa na maana binaadamu hatoshi kuangaza habari za Mungu.
 
Sina maana hiyo uliyoelewa wewe,nachokusudia ni kwamba Mungu anahusishwa na mambo mengi hivyo habari za kuhusu Mungu ni pana si suala la aliyeumba au kutengeneza binaadamu tu. Sikuwa na maana binaadamu hatoshi kuangaza habari za Mungu.

Basi kama ni hivyo kwako hakuna sababu ya wewe kuwa na wasisi juu ya dhana zangu wala za mtoa mada

Ni taratibu tu za kuruhusu akili na kufikiria nje ya mipaka waliyojiwekea watu kwa maslahi yao

Labda cha kuepuka kwako na watu wa dini ni kuzunguzia dhana kama uhalisia na ndio maana waelewa waliamua kuyaweka mafikirio ya namna hiyo katika kundi la imani ili mtu asipate bugudha kwa kile anachokiamini

Mimi kusema mungu kafa au kasafiri ni dhana zangu binafsi ila ukitaka kuogelea kwenye bahari yangu ya dhana naweza kujaribu kukushirikisha ila nakuhakikishia ni za uchizi kuliko hizo nilizotangulia kutaja zitakazokupelekea kuhisi nawehuka na nataka kukuambukiza wehu.!

Ni heri ubaki na imani yako
 
Nilichotaka kujua ni kwamba Huyo Mungu unayemjengea hizo dhana unamkusudia Mungu yupi au unakusudia nini unaposema Mungu wakati unapoeleza dhana zako?

Tunajadiliana tu hapa kuna wengi huwa wanajifunza mambo mengi tu bila kujari sie tunaojadili tunachukuliana vp,najua hata wewe unaona watu wa dini ni kama wamewehuka lakini hiyo haizuii kuacha kujadiliana.
 
Nilichotaka kujua ni kwamba Huyo Mungu unayemjengea hizo dhana unamkusudia Mungu yupi au unakusudia nini unaposema Mungu wakati unapoeleza dhana zako?
Nakusudia yule mungu wanayemvutia picha watu wa dini kwa kufikiri kwao

Unajua ni nini.! Hata wao wenyewe hawajafikia mkataa wa muonekano wa huyo mungu.!

Wengine wanadhani ni roho iliyo kila mahali na wengine wanaona ni kama mtu mmoja aliyekaa eneo moja lakini mweke koneksheni ya maeneo yote ya ulimwengu

Kwaiyo nikiwa naeleza dhana zangu hizo elewa zinajinyumbulisha kote huko

Nikisema kafa au kasafiri tambua naeleza katika kimoja chenye kuonekana

Lakini nikimuelezea huyo mungu katika namna yin & yang au lingam & yoni tambua naelezea katika kile kisichoonekana kama nguvu fulani yenye kutenda kinyume kuwezesha maisha

Ila usisahau kuwa zote ni dhana
 
Ndio maana nikasema Mungu anahusishwa na mambo mengi ni zaidi ya kuhusishwa na kuumba/kutengeneza binaadamu.

Labda nikuulize kwamba ni yepi unadhani yangepaswa yawepo au unadhani hali ingetakiwa iweje kama kweli Mungu angekuwepo?
 
Labda nikuulize kwamba ni yepi unadhani yangepaswa yawepo au unadhani hali ingetakiwa iweje kama kweli Mungu angekuwepo?
Nadhani zile ahadi za pepo au paradiso zingekuwa zinapatikana hapa duniani ingekuwa ni heri sana kwa watu wote

Hata kama asingeonekana na kujificha bado kungekuwa na kiashiria cha kujali kwa watu wote na kupelekea watu kumuamini

Lakini kwa kutokujali na kujificha wakati walimwengu wanamuhitaji, kunapelekea watu kutoona thamani yake na maisha kwa ujumla, hivyo kupelekea kuzua maswali mapya kichwani mwao juu ya uhusika wake

Kuwa mungu na kutengeneza maisha yasiyo na uwiano kama haya ni kukosea adabu ufahamu ni heri angekaa kimywa bila kufanya lolote lile nina hakika angeeleweka kuliko upuuzi kama huu halafu unasema umetokezwa na mungu muweza yote.!?

Na ndio maana waliotangulia kuyafahamu haya wakawa na mafikirio mapya ya dhana kama hizi ili kuwa na misingi thabiti juu ya nini kinaendelea kwenye maisha haya yasiyo na maana

Kwamba vipi.. Yawezekana kuna wahuni kutoka anga za mbali wanatufanyia kamchezo.?
 
Ukiangalia vizuri swali nililokuuliza mwishoni nimemalizia hivi "..kama kweli Mungu angekuwepo" nikiwa na maana ya kwamba hayo mambo kutokuwepo kunafanya madai ya uwepo wa huyo Mungu kuwa si za kweli au kutowezekana kuwepo. Sasa ulichoeleza wewe kama kujificha kwa Mungu na watu kumuhitaji,sijui ahadi za pepo kuwepo duniani sidhani kwa hayo mambo tunaweza kutumia kufanya tuone Mungu hakuna.

Ulichoeleza ni kama malalamiko kwa Mungu na ni kitu ambacho hata mwenye kuamini Mungu hufanya ingawa hana shaka na imani yake juu ya kuwepo Mungu.
 
Jitahidi kusoma na kuelewa

Sasa nimejibu na wewe huoni kingine zaidi malalamiko unataka nifanye vipi ili uone nimejibu.!

Au ulitaka nikuambie maji yakauke aridhini yawepo angani ili papa na nyangumi tuwaone live bila chenga, fisi simba kwa jamii yao wasiwepo maana wanatumalizia kitoweo,wazungu nao watoweke maana ni wakorofi_hapo ndio ningetosheleza kiu yako.?
 

Mtoa mavi unaumiza kichwa bure. Alliens ni wachina ndio maana ukiwatazama Alliens wote wanafanana Kama walivyo wachina.

# mods badilisheni hapo Juu, sijamaanisha MTOA MAVI, nimemaanisha MTOA MADA.
 
Hivyo midhahabu ile ya kina Mansa Musa, Mwanamutapa, imehifadhiwa wapi? Nilisoma mahali kwamba mashimo ya dhahabu ya kina Mwanamutapa ni ya kustaajabisha sana pengine yalipaswa yawe kwenye maajabu ya dunia.

Sent from my BLL-L21 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…