Proof of God

Duh! Hayo umetoa wapi? Embu rudi huenda hukunielewa. Yote niliyouliza ni kutaka kujua iwapo ubaya ulikuwepo kabla ya dhambi kutokana na uchaguzi wa kutokutii kwa binadamu na shetani.
sio ubaya ni tulipewa uhuru wa kuchagua, kumtii Mungu au kuto mtii.
 

 
Tukauchagua ubaya tusioufahamu? Kutokutii ni jambo baya si ndio?
One question, unakubali uwepo wa Ufahamu Mkuu ambao kutoka kwake ndio tunapata ufahamu na kweli?

Au ufahamu wetu ni matokeo ya ajali ya atomi kugongana gongana?
 
Mmenikumbusha scene ya kwenye The Croods, don't eat the bananas

 
One question, unakubali uwepo wa Ufahamu Mkuu ambao kutoka kwake ndio tunapata ufahamu na kweli?

Au ufahamu wetu ni matokeo ya ajali ya atomi kugongana gongana?
Kugongana ni ajali. Ajali huaribu haiweki vitu katika mpangilio. Mfumo wa sayari, anga, maumbo na nguvu zote tunazoiona na tusizoziona sio ajali. Unless una tafsiri tofauti ya kugongana gongana.
 
Kutokutii si ni jambo baya? Mtoto anayekosa utii anafanya jambo zuri au baya?
Unajua kuna wengine wanasoma hilo simulizi kama metaphor kuelezea kuwa hii hali yetu, ya kutambua uwepo wa viwango vya Maadili, hali yetu ya kutofurahishwa na uovu wa wengine, ya kutamani kufanya mema, lakini pia hali ya sisi wenyewe kushindwa kuishi kulingana nayo mf. Kutompenda jirani kama wewe mwenyewe n.k, jumlisha na masimulizi ya wazee wetu wa zamani wa kuwepo na watu waadilifu hapo mwanzoni,

yote haya yanaashiria kuwepo kwa anguko la binadamu hapo zamani.

Lakini nimekuelezea na uelewa wa Wahindu kuwa sisi ni vijisehemu vya Ufahamu wa Mungu vivyojitokeza, yaani sisi ni Mungu aliyechukua umbo la viumbe hai kwenye ulimwengu ulio conditioned ambao aliutokeza pia (aliuumba), uovu kwenye ulimwengu huu ni asili, ambao unatokea kwa sababu ya ignorance (kutokujua), na lengo kuu la sisi kutokea ni ku experience maisha kisha kurudi kwenye asili yetu ya ukweli yani kuwa Mungu, ambapo kurudi pia kuna conditions, ndo hapo viwango vya maadili vinatokea...na mengine
 
Reactions: Tsh
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…