Propaganda ni mbaya sana, imepotosha Watanzania

nditolo

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2011
Posts
3,731
Reaction score
4,271
Niende Moja kwa Moja kwenye lengo.

Tangu 2007 baada ya Serikali kuanguka kutokana na matokeo ya tume huru iliyoongozwa na kaka yangu Mwakyembe, watanzania waliaminishwa Lowasa ni mbaya sana.

Ikafikia hata baadhi ya matamko kutoka kwenye vinywa vya watoto wa viongozi wa kipindi hicho (Ridhiwani) kuwa iwe Jua au mvua hawezi kuwa Rais.

Kufika 2015 katika harakati za kutafuta mgombea kupitia CCM, Mzee akakatwa makusudi Ili kuudhihirishia umma kuwa Lowasa hafai.

Hapo ndipo sura ya taifa la Tanzania likabadirika.

Tukashuhudia sio propaganda tu Bali mpaka mauwaji kwa wenye hoja tofauti.

Watanzania tukagawanywa vibaya katika kabila, Kanda, mpaka Koo.

Nchi imepitia kipindi kibaya sana kuwahi kushuhudiwa tangu uhuru.

Tuna makovu makubwa sana.

Lakini Kuna mwanga nimeamza kuuona sasa[emoji116][emoji116]

Moyo wangu umefarijika sana.

Lakini mama ana kazi kubwa ya kufanya.

Kuwaaminisha watanzania kuwa zile hazikuwa siasa za kistaarabu.

Kupigana, kutekana, kuuwawa kubambikia kesi
Kuwaaminisha watanzania kuwa wapinzani ni wazalendo kuliko Wana CCM.

Tuendelee kuomba Mungu hii Suluhu inayofanyika itimie. Maana kundi la akina Sabaya lipo Bado na Lina nguvu pia.

Ahsante sana
JamiiForums1943670800.jpg
Screenshot_20220217-060434.jpg
JamiiForums62396982.jpg

Screenshot_20220217-060434.jpg
 
Tuendelee kuomba Mungu hii Suluhu inayofanyika itimie. Maana kundi la akina Sabaya lipo Bado na Lina nguvu pia.[emoji1534][emoji1533]
 
Kina Kingai,Mahita,Swila ,J4 bado wapo na Prof wa Meru arudishiwe mpunga wake J4 alio uchukua
 
Kulikuwa na organization fulan isiyokuwa rasimi kwenye vyombo vya ulinzi ambayo ilikuwa ni ya watu wa Kanda ya ziwa.

Hawa walikuwa informers na mahususi kwa yoyote anayeonekana mpenda haki na hashabikii uonezi waliokuwa wanafanyiwa upinzani hasa tangu Tundu Lissu alivyopigwa risasi.

Tuombe Mungu, Mama afanikishe haya maridhiano Ili kuwepo na mizani sawa kwa Kila chama.

Pia police department wapewe seminar waelewe kuwa wao ni civil servants na sio Wana CCM (police CCM)
 
Chadema ndio chanzo cha Lowassa kuchukiwa propaganda ilianza pale mwembe yanga labda ulikuwa hujaziliwa!
 
Mengine yakikupita sio mbaya. Huwa yanaficha aibu na kulinda heshima yako.
Mlishindwaje kimfungulia mashtaka wakati mlikuwa na mna dola?
 
Zile zilikuwa siasa za kawaida sana. Na ndio maana Mzee alipotoswa CCM akaenda chadema. Na akaaminika na kuingiza wabunge na kura halali kuzoa.

Kumzuia Lowasa kukatuletea shetani.

Tumechafuka mpaka Leo. Chukulia wewe ndio ungekuwa Mama Samia!! Yaani ni kazi ngumu sana kusafisha madoa ya DAMU
 
Chadema ndio chanzo cha Lowassa kuchukiwa propaganda ilianza pale mwembe yanga labda ulikuwa hujaziliwa!
Na aliyeanzisha na kutunga propaganda ile na kumpatia "rais wa mioyo ya baadhi ya watu" ili aisambaze wakati huo ni Lissu. Lissu alikiri kufanya jambo hili hadharani.
 
Tuendelee kuomba Mungu hii Suluhu inayofanyika itimie. Maana kundi la akina Sabaya lipo Bado na Lina nguvu pia.[emoji1534][emoji1533]
Na kuna kundi la wafaidika wa fedha za michango ya kesi , kesi ikiisha hawana kazi copy, MMM, Maria na wengineo
 
Mungu aendelee kunsaidia . Kiukweli kabisa hakuna urafiki wa paka na panya hata siku moja.
Miaka ikienda Sana kwa bahati mbaya hutokea either panya akawa paka ama aidha paka akaendelea kua paka.
Hao panya kuwakaribisha nyumbani ghalani ni mtihani. Hawana shukrani hao
 
Mama amekuwa mkombozi. Lile kundi la marehemu lingetusumbua sana
Hakika.

Lile kundi lilitusumbua sana. Sasa hivi watu hawauawi, umeme haukatiki, ajira bwerere, hakuna case za kubambika.

Hakuna mfumuko wa bei, hakuna kukimbizana na TRA wala Policcm, mikutano ya kisiasa imeruhusiwa, bei za mafuta na sukari zimeshuka. Gharama za umeme ni rafiki kwa mwananchi wa kawaida.

Sasa hivi hakuna ufisadi wowote, hela zimekuwa nyingi mtaani tunaziokota tu, hakuna tozo, machinga wanafanya kazi kwa uhuru, hakuna kuungua masoko, n.k.

Yaani tulichelewa kumpata mama.
 
Niende Moja kwa Moja kwenye lengo.

Tangu 2007 baada ya Serikali kuanguka kutokana na matokeo ya tume huru iliyoongozwa na kaka yangu Mwakyembe, watanzania waliaminishwa Lowasa ni mbaya sana.

Ikafikia hata baadhi ya matamko kutoka kwenye vinywa vya watoto wa viongozi wa kipindi hicho (Ridhiwani) kuwa iwe Jua au mvua hawezi kuwa Rais.

Kufika 2015 katika harakati za kutafuta mgombea kupitia CCM, Mzee akakatwa makusudi Ili kuudhihirishia umma kuwa Lowasa hafai.

Hapo ndipo sura ya taifa la Tanzania likabadirika.

Tukashuhudia sio propaganda tu Bali mpaka mauwaji kwa wenye hoja tofauti.

Watanzania tukagawanywa vibaya katika kabila, Kanda, mpaka Koo.

Nchi imepitia kipindi kibaya sana kuwahi kushuhudiwa tangu uhuru.

Tuna makovu makubwa sana.

Lakini Kuna mwanga nimeamza kuuona sasa[emoji116][emoji116]

Moyo wangu umefarijika sana.

Lakini mama ana kazi kubwa ya kufanya.

Kuwaaminisha watanzania kuwa zile hazikuwa siasa za kistaarabu.

Kupigana, kutekana, kuuwawa kubambikia kesi
Kuwaaminisha watanzania kuwa wapinzani ni wazalendo kuliko Wana CCM.

Tuendelee kuomba Mungu hii Suluhu inayofanyika itimie. Maana kundi la akina Sabaya lipo Bado na Lina nguvu pia.

Ahsante sanaView attachment 2121637View attachment 2121638View attachment 2121640

View attachment 2121639
Siasa Ni mbaya sana hapa kwetu.

Imefanya watu wamekuwa misukule wa kutupwa wa wanasiasa.

Mpaka sasa sijaona watu wakishukuru eti kwasababu matatizo yao yamesikilizwa.

Kuna nyumbu ambao yaani ili uonekane uko vizuri Ni lazima uwasikilize wao.

Usipowasikikiza wao basi kila kitu kitakachoendelea wataona hakuna unachofanya.

Jana Lissu kaongea matatizo yao tu wanasiasa na ya kwake tu.

Haya wale mazwazwa wanaodhani matatizo yao maji, umeme, ajira, ardhi, masoko, Kilimo watafute na wao sehemunya kusemea.

KILA mtu apambane na hali.
 
Kulikuwa na organization fulan isiyokuwa rasimi kwenye vyombo vya ulinzi ambayo ilikuwa ni ya watu wa Kanda ya ziwa.

Hawa walikuwa informers na mahususi kwa yoyote anayeonekana mpenda haki na hashabikii uonezi waliokuwa wanafanyiwa upinzani hasa tangu Tundu Lissu alivyopigwa risasi.

Tuombe Mungu, Mama afanikishe haya maridhiano Ili kuwepo na mizani sawa kwa Kila chama.

Pia police department wapewe seminar waelewe kuwa wao ni civil servants na sio Wana CCM (police CCM)
Pagumu hapo bila katiba mpya
 
Mengine yakikupita sio mbaya. Huwa yanaficha aibu na kulinda heshima yako.
Mlishindwaje kimfungulia mashtaka wakati mlikuwa na mna dola?
Kwani nyie mlishindwa vipi kumfungulia ,mbona kubenea kamfungulia makonda nyinyi shida iko wapi?
 
Back
Top Bottom