Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
wanajamii naombeni msaada, kuhusu Tax Law hasa kwenye ishu ya property, je ni kweli kwamba mstaafu kwa hapa tanzania yupo exempted kulipa kodi kwa mapato yatokanayo na rent ya nyumba yake aliyopangisha ?
Kwanza naona kama vile unachanganya vitu viwili hapo, income tax (kodi ya mapato) na property tax (kodi ya majengo) ni kodi mbili tofauti na zinaongozwa na sheria mbili tofauti. Property tax inakusanywa na local govts (kwa sasa wamewapa hiyo kazi TRA kwa DSM) na Income tax inakusanywa na TRA kwa ajili ya central govt. Either way, wastaafu hawapo exempted (chukulia kwa mfano mstaafu ana nyumba arobaini za kupangisha....kweli asamehewe kodi kwa sababu tu ni mstaafu!?).
Mbali na kodi ya majengo (property tax), pia kuna kodi nyingine inaitwa kodi ya pango la ardhi (land rent). Kodi hii hutozwa kwa viwanja ambavyo vimepimwa na kuandaliwa hati ya kiwanja. Inaitwa kodi ya pango la ardhi kwa sababu Sheria yetu (Na. 4) ya Ardhi ya mwaka 1999 sehemu ya 4 (Land Act No. 4 of 1999, section 4) inasema ardhi yote ni mali ya umma na amepewa rais kama mdhamini. kwa hiyo mtu mmoja mmoja anapopata ardhi ni kwamba anapangishwa kwa kipindi cha miaka 33, 66 au 99. na kwa kipindi chote hicho mtu aliyepewa ardhi atatakiwa kulipa kodi ya pango la ardhi pamoja na kutimiza masharti mengine ya umiliki.Nashukuru wadau..kwa muongozo wenu...Viva jamiiforums...!!!!
Mkuu SMU, hizi rent tunazozilipa kwa wenye nyumba wetu uswahilini zinatakiwa zitozwe kodi kwa utaratibu gani? Manake naona kama serikali haikusanyi kodi huku uswahilini kwetu.