Prosper Mbuba: Rio ameleta manufaa mengi sana, ameangalia goli la Chama, ametembelea serengeti. Hayo ndio mambo tuyapendayo vijana

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Ukimsikiliza huyu jamaa wakuitwa Prosper Mbuba utadhani kama anamwaga sifa za kichawa kwa Makonda au Serikali lakini kiuhalisia ni anafanya mzaha wa kebehi kabisaa

Yani amezungumza ujio wa Rio Ferdinand nchini Tanzania kuwa una manufaa mengi sana ikiwemo kuliona goli la Chama na kuifahamu Simba na kusema hayo ndio mambo tuyapendao vijana, lakini pia ametembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Soma Pia: Baada ya Drogba, Makonda amualika Nahodha zamani wa Manchester United Rio Ferdinand kuja Tanzania

Lakini pia akatumia mzaha mwengine kwa Gerson Msigwa kwa kusema semaji letu ambalo alitaki kutukanwa na ukitukana tu utakamatwa. Ambapo katika maelezo yake akimnukuu Msigwa amesema Rio amekuja kwa sababu ya mahusiano yake na Makonda na si kwa fedha za seikali lakini pia kwa maoni yake amesema hata waandishi wa habari nauli za kwenda Dodoma wamejilipia

Ila enjoy mwenyewe kumsikiliza jamaa anafikisha ujumbe wake kwa namna tofauti. Binafsi niemjoy sanaa

Your browser is not able to display this video.
 
Rio kama Rio yaani
Kweli serikali imefilisika kimawazo
 
well done and welcome again Rio 🐒
 
hahahahaa huyu jamaa noma, usipokua na akili timamu utasema chawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…