Protein supplements, protein shakes

Protein supplements, protein shakes

gasgas

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2015
Posts
1,092
Reaction score
986
Habari wanajamvi, mimi ni kijana wa miaka 21, ninafanya mazoezi ya weight lifting lengo likiwa ni kujenga mwili mzuri ambao upo fit. Sasa nasumbuliwa na tatizo moja, ni kwamba mimi ni mwembamba sana, na kwa kipimo cha BMI nakaribia kushuka kwenye underweight.

tangu nimeanza mazoezi nimeona faida kidogo sema nahisi narudishwa nyuma na kutokupata calories za kutosha

Najitahidi kula sana na kwa wingi ila ki-ukweli chakula ninachoweza kununua hakifikii ile idadi ya calories ninazohitaji kwa mwili wangu illi niweze kufikia uzito na mwili niutakao.

hivyo basi naulizia protein supplements, protein shakes ziweze kujalizia pale ambapo chakula hakitoshi ili malengo yafikiwe.

lengo ni kuingiza mwilini calories 3000-3500 za clean protein.

kama unafahamu wapi ntapata hizi protein supplements ntashhukuru sana ukinisaidia, kama haufahamu tafadhali naomba uache wanaofahamu washirik

usiku mwema!
 
Asante kwa ushirikiano nimefanikiwa kuzipata
 
Mwenzio juzi kaanguka msikitini. Kisa moyo umetanuka
 
Mkuu nakushauri kabla ya kuanza kutumia uombe ushauri zaidi kwa daktari kama zina side effects uzijue.
 
Mwenzio juzi kaanguka msikitini. Kisa moyo umetanuka

Kuna tofauti kubwa sana. Sio supplements zote ziko sawa
Kuna
1. Anabolic steroids hizi ndizo zina side effects hizo ulizotaja hapo kwa sababu steroids zina mineralcorticoid effect, zinasababisha figo kuchukua Sodium kwa wingi na hivyo kusababisha water retention, na hivyo kuongeza kiwango cha damu mwilini na moyo inabidi ukue (hypertrophy) ili kuweza kupump damu iliyoongezeka (demand kubwa) na matatizo mengine yanayofuata

2. Mass gainers na protein shakes
Hizi ni protein za kawaida tena healthy kama vile whey protein, soy protein zinazopatikana kwenye vyakula lakini zimetenenezwa katika lishe ambayo inamsaidia mtu kuzipata katika ujazo mkubwa na hivyo husaidia kwa wale wenzangu na sisi ambao kutokana na hali ilivyo hatuwezi kupata protein za kutosha kwenye diet (calories/kg) kuweza kufikia kiwango kinachotakiwa kwa ajili ya kujenga mwili.

Nyingi kati ya hizi huwa zina calories nyingi per serving 700 na kuendelea
 
Asante mkuu. Usihofu juu ya hilo
 
Habari wanajamvi, mimi ni kijana wa miaka 21, ninafanya mazoezi ya weight lifting lengo likiwa ni kujenga mwili mzuri ambao upo fit. Sasa nasumbuliwa na tatizo moja, ni kwamba mimi ni mwembamba sana, na kwa kipimo cha BMI nakaribia kushuka kwenye underweight.

tangu nimeanza mazoezi nimeona faida kidogo sema nahisi narudishwa nyuma na kutokupata calories za kutosha

Najitahidi kula sana na kwa wingi ila ki-ukweli chakula ninachoweza kununua hakifikii ile idadi ya calories ninazohitaji kwa mwili wangu illi niweze kufikia uzito na mwili niutakao.

hivyo basi naulizia protein supplements, protein shakes ziweze kujalizia pale ambapo chakula hakitoshi ili malengo yafikiwe.

lengo ni kuingiza mwilini calories 3000-3500 za clean protein.

kama unafahamu wapi ntapata hizi protein supplements ntashhukuru sana ukinisaidia, kama haufahamu tafadhali naomba uache wanaofahamu washirik

usiku mwema!

helo mkuu niaje? me mwenyewe ninatafuta whey protein,hivi umezipata wap ? na kwa bei gan?
 
kuna jamaa anafanya kazi gym ya sparta anauza bei kuanzia 180,000 kopo lina kilo mbili na kuendelea
 
Gasgas karibu Kwa ushauri 0752666283 kwani kuna pack special kwa Wana mazoezi ni nzuri Sana na wengine wote wenye uhitaji.
 
Naona itakuwa vyema ukaelezea humu kwa sababu ni watu wengi wanatafuta hizo kitu.

Unatoa supplements gani, kwa bei gani? Kiasi gani? Napata calories ngapi per serving?

Kwa mfano mimi niliyoipata wanauza 180,000, kopo lina uzito wa 5 pounds, 700 calories per serving. Ya kwako iko vipi mkuu?
 
Nashukuru mkuu. Ya kwangu inaitwa Forever lite ultra vanilla shake mix hii Ina 18.5 oz Ni sawa na 524g unapata 4 calories per gram ina maana ukimaliza kopo inakuwa 2096, bei yake ni Tsh 70,500.00 inasaidia kujenga mwili na virutubisho kamili.
Nyingine inaitwa ARGI+ inasaidia misuli kuwa imara na yenye nguvu na kuimarisha mifupa. Hii Ina 10.6oz ni sawa na 300g bei yake ni 140,500.00
 
Mimi huwa najarib kupiga misosi ya kutosha hasa yenye protein zaid, thank Mungu kanipa mwili poaa nikigusa Gym kidgo najaaa hatari so hapa na avoid gym kukuza mwili bt napiga tizi ni ripped
 
Poa! Ntakucheki nikihitaji
 
Mimi huwa najarib kupiga misosi ya kutosha hasa yenye protein zaid, thank Mungu kanipa mwili poaa nikigusa Gym kidgo najaaa hatari so hapa na avoid gym kukuza mwili bt napiga tizi ni ripped

Wengine wetu ni hardgainers, inahitaji zoezi jingi kwa muda mrefu na chakula juu ili kuweza kuongezeka
 
Mkuu gasgas hizo supplements zinauzwa wapi??
 
Back
Top Bottom