Kuna namna nyingi ya kutunza vyeti vyako viwe ktk hali ya usalama. Kwa miaka mingi nimetunza vyeti vyangu ndani ya bahasha ambalo ninahakikisha halikunjwi na ninaweka kwenye sanaduku chini kabisa. Kama sanduku huna hata kabatini unaweza ukaweka. Nilipopata kazi nikanunua briefcase. Tena nakumbuka muuza duka alinishangaa mwanamke kunua briefcase. Nikaweka kwenye briefcase. Kwa sasa ninazitunza kwenye safety deposit box kwenye benki. Cha muhimu vitunzwe mahala pasipo na unyevunyevu. Kuhusu provisional results au transcript. Unapaswa uchukue copy za kutosha. Ni muhimu sana kuhakikisha unawekeza ktk kutafuta kazi. Pia ukikosa kazi ni haki yako kwenda kudai copy zako za vyeti na provisional results maana hazina kazi tena pale ulipoombea kazi na ukakosa. Kampuni zingine zina tabia za kuwarudishia documents watu waliokosa kazi. Kumbuka huwezi kupata kazi/kitu chochote kizuri bila investment.