PSG kumtambulisha Neymar kwa ‘mbwembwe’ Jumatano

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
12,320
Reaction score
11,327
Kwa mashabiki wa klabu ya Barcelona huenda wasiamini tetesi za mshambuliaji wao Mbrazil, Neymar Jr kuwa ameitosa klabu yake na kuhamia kwa matajiri wa Ufaransa, Paris Saint-Germain, ukweli ni kwamba dili hilo ni asilimia 98 limeshatiki kinachosubiriwa ni masaa tu atangazwe.

Kwa mujibu wa magazeti makubwa nchini Ufaransa kama L’Équipe na Europe 1 yametangaza kuwa Neymar leo jumanne anaenda Doha, Qatar kuonana na Rais wa klabu hiyo Nasser Al-Khelaifi na kufanyiwa vipimo vya afya.

Zoezi la kumtambulisha na kumtangaza Neymar linatarajiwa kufanyika kesho, jumatano tar 2 Agosti kwa mbwembwe ndani ya jiji la Paris nchini Ufaransa ambapo maelfu ya mashabiki wa klabu hiyo watahudhuria kwenye uwanja wa klabu hiyo.

Kwa mujibu wa gazeti la L’Équipe taarifa zinaeleza kuwa viongozi wa klabu hiyo wapo kwenye mazungumzo na Meya wa jiji hilo kuomba kibali cha kuweka picha kubwa ya Neymar kwenye mnara maarufu zaidi duniani ulio katikati ya jiji hilo ujulikanao kwa jina la Eiffel kama walivyowahi kufanya kwa Zlatan Ibrahimovic walivyomsajili akitokea Barcelona.

Uhamisho wa Neymar kutoka Barcelona umeripotiwa kuwa ni wa Euro Milioni 193 na kama itatokea utakuwa ndio usajili wa ghali zaidi duniani kuwahi kutokea katika historia ya mpira wa miguu.

Hata hivyo taarifa hizo za Neymar kuhama Barcelona zinashika kasi kwa kile kinachoonekana kuwa klabu hiyo imeshindwa kumlipa baba yake mzazi na Neymar, Neymar Sernior ambaye ndiye meneja wake kiasi cha Euro Milioni 26 kama masharti ya mkataba yalivyoeleza.

Katika mkataba alioingia na Barcelona akitokea Klabu ya Santos ya Brazil, unaeleza kuwa kama Neymar akiongeza mkataba mpya na Barcelona, basi baba yake huyo ambaye ni meneja wake anapaswa kulipa kitita cha euro milioni 26.

hapa alikua ndio anatoka DUBAI dogo kuonana na sheikh,..usajili wake utakua zaidi ya bilioni 500 na ushee za kitanzania....ni pesa juu ya pesa tu hamna namna.
 
hapa alikua ndio anatoka DUBAI dogo kuonana na sheikh,..usajili wake utakua zaidi ya bilioni 500 na ushee za kitanzania....ni pesa juu ya pesa tu hamna namna.
neymar mbona alikuwa china kwaajili ya promotion na leo anarudi barc kesho mazoezini kama kawa na barcelona au unamzungumzia neymar sr ndio aliyeenda dubai?
 
akibaki barca atacheza nyuma ya kivuli cha messi bora aondoke
Na mimi napenda asepe tu akajitengenezee jina PSG amwache messi tu pale ndo anaabudiwa kama mungu

What goes around always comes around
 
Hela mkuu...hela zinamwasha tajiri wa psg

What goes around always comes around
Labda wameshafanya mahesabu yao wakaona watauza jezi za kutosha kufidia japo 50%. Ule mpunga hata kwa viwango vya Ulaya sio wa spotispoti.
 
Labda wameshafanya mahesabu yao wakaona watauza jezi za kutosha kufidia japo 50%. Ule mpunga hata kwa viwango vya Ulaya sio wa spotispoti.
Haha kabisa mkuu.

What goes around always comes around
 
Not worth all that money. PSG are fools
[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] consultant umesemaaaaaa[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38]
neymar mbona alikuwa china kwaajili ya promotion na leo anarudi barc kesho mazoezini kama kawa na barcelona au unamzungumzia neymar sr ndio aliyeenda dubai?
 
Sikutegemea huyu aondoke BARCA sijui wamemuudhi nini mpaka akaamua kuondoka.
 
Labda wameshafanya mahesabu yao wakaona watauza jezi za kutosha kufidia japo 50%. Ule mpunga hata kwa viwango vya Ulaya sio wa spotispoti.
mpunga unatoka kwenye serekali ya Qatar (ndio wamiliki wa psg). hiyo kwao ni hela ndogo sana hata wakipata hasara wao shida yao wanataka neymar aitangaze nchi yao vizuri kabla ya world cup 2022.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alaa inawezekena aise

What goes around always comes around
 
Sikutegemea huyu aondoke BARCA sijui wamemuudhi nini mpaka akaamua kuondoka.
Naona update kwamba Barca wanamtaka Di Maria ili akaungane na messi na suarez sasa kwaio inamanisha kwamba Neymar anaweza sepa mda wowote kuanzia sasa

What goes around always comes around
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…