PSG yamweka sokoni Cavani ili kumnasa Sanchez

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Paris, Ufaransa.Wakati UEFA ikiwahemea shingoni kutokana na kuvunja kanuni za fedha (FFP), Paris Saint-Germain imeripotiwa kuwa wapo tayari kuuza mshambuliaji wake Edinson Cavani ili kujihakikishia kumnasa nyota wa Arsenal, Alexis Sanchez msimu ujao.

Miamba hiyo ya Ufaransa ‘Ligue 1’ kwa sasa wapo chini ya uchunguzi kutoka Shirikisho la Soka Ulaya baada ya kuvunja rekodi ya uhamisho kwa kununua mkataba wa Neymar pamoja na kumchukua kwa mkopo Kylian Mbappe.

Wakati hilo likiwa halijakaa sawa gazeti la michezo la Ufaransa la Le Parisien limeripoti kuwa mataji wa Qatar wanajianda kuanzisha mazungumzo na Sanchez, ambaye atakuwa huru baada ya mkataba wake kumalizika mwakani.

Pia inaaminika kuwa PSG ilikuwa na mawasiliano na nyota huyo Arsenal msimu huu lakini hawakufikia makubaliano. Kutokana na hali hiyo PSG sasa watalazimika kuuza Cavani ili kuondoa thamani euro 80milioni inayotakiwa katika vitabu vyao vya fedha.



mwananchi
 
Tetesi ya usajili mwezi wa 10

Hii ni uongo tu kuuza magazeti
 
Khaaaah! Mpaka huku pia upo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…