Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umesema kila mwezi huwalipa Sh. bilioni 60 wastaafu wa mfuko huo.
Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Mfuko huo, James Mlowe, alisema fedha hizo hulipwa wastaafu 150,000 kwa mwezi.
Aidha, alisema Mfuko huo unalipa zaidi ya Sh. bilioni 120 kila mwezi mafao mengine ikiwamo ya uzazi, ukosefu wa ajira, mafao ya ugonjwa, ya kifo na wategemezi.
Mlowe alisema hayo jana alipotembelea ofisi za magazeti ya Nipashe na The Guardian zilizopo Mikocheni, jijini Dar es Salaam ikiwa ni ziara ya kufahamiana na kujenga uhusiano.
Akizungumzia jumla ya malipo yanayotolewa na Mfuko huo, alisema kila mwezi ni zaidi ya Sh. bilioni 180.
Meneja huyo alisema baada ya kuunganishwa kwa mifuko ya LAPF, PSPF, GEPF na PPF na kuwa mfuko mmoja wa PSSSF mwaka 2018, ulipitia changamoto mbalimbali ikiwamo kukosa pesa za uendeshaji kwa sababu hawakuwa na kipindi cha mpito cha kujijenga bali walianza utekelezaji moja kwa moja kwa kulipa mafao ya wastaafu.
“Tulipounganisha mifuko tulikuwa na deni la Sh. trilioni moja ya malipo ya mafao kwa wastaafu, kwa hiyo hiyo ilikuwa ni changamoto ya kwanza kwenye mfuko,” alisema.
Aliitaja changamoto nyingine iliyowayumbisha katika kulipa madeni hayo ni kulazimika kulipa madeni ya wastaafu wa zamani yaliyotakiwa kulipwa na Hazina, ambayo fidia yake haikulipwa kwa wakati.
“Bahati mbaya serikali haikufanikiwa kulipa kwa wakati hiki kiasi ambacho mwanachama alitakiwa kulipwa, kitendo kilichosababisha deni hili kukua hadi kufikia Sh. trilioni 4.6. Hii ilisababisha PSPF ikayumba sana, sasa tulipoungana PSSSF ikaibeba hiyo shida,” alifafanua.
Alisema anamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo ya uongozi wake alitoa hatifungani ya Sh. trilioni 2.17 kwa ajili ya kulipia deni hilo na kuahidi baada ya miaka mitatu atamalizia kiasi kilichobaki.
“Tunashukuru jitihada za serikali katika kuiokoa PSSSF kwa sababu kiukweli tuliungana, lakini bila hiyo tayari tulikuwa tunarudi chini, kwa sababu unakuwa unalipa zaidi ya unachokipata,” alisema.
Vilevile, Mlowe alisema hadi kufikia Februari, mwaka jana walifanikiwa kulipa asilimia kubwa ya wastaafu.
Wastaafu hao wanawalipa kutokana na vyanzo vyao vikubwa vya mapato ikiwamo michango ya wanachama ya kila mwezi wanayokusanya kwa waajiri na uwekezaji katika majengo ya kibiashara alioutaja unafikia ni Sh. trilioni 7.8.
Aidha, Mlowe alisema wamerahisisha huduma kwa wanachama kwa kufungua ‘application’ kwenye simu inayomwezesha mwanachama kupata huduma zote bila kwenda kwenye ofisi zao.
“Zamani ilikuwa mwajiri akitaka kuleta michango ya mwezi husika atalazimika kuja ofisini kwetu, ajaze fomu za kulipia, kisha aende benki akapange foleni, inachukua muda na watu sasa wana mambo mengi ya kufanya, ndio maana tumekuja na hizo application,” alifafanua.
Alisema kuunganishwa kwa mifuko hiyo kumepunguza gharama za uendeshaji kutoka Sh. bilioni 128 kwa mwezi hadi Sh. bilioni 68 hali inayoongeza manufaa kwa wanachama.
Mfuko wa PSSSF una jumla ya wanachama 810,000.
Nipashe