Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Kusoma zaidi alichoandika Mdau bofya hapa ~ Serikali tunaomba muitazame upya PSSSF Branch ya Arusha, huduma ziboreshwe
UFAFANUZI KUHUSU MADAI YA TATIZO PSSSF ARUSHA
Kwenye ukurasa wa Jamii Forums, kuna taarifa yenye kichwa "Kuna Tatizo PSSSF Arusha." Taarifa hiyo inadai kuwa wanachama watatu wamefuatilia mafao yao kwa muda mrefu, na wawili kati yao wanasemekana kufariki dunia wakiwa bado wanashughulikia mafao yao kupitia Ofisi yetu ya Kanda ya Kaskazini, jijini Arusha.Awali ya yote, tunapenda kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, na marafiki wa wanachama wetu iwapo kweli wapo waliopoteza maisha wakiwa katika mchakato wa kufuatilia mafao yao.
Aidha, uchambuzi wa madai yaliyotolewa unaonyesha kuwa yamejikita zaidi kwenye dhana ya kufikirika ambayo haiwezi kusaidia mlalamikaji wala Mfuko katika kutatua tatizo lolote endapo lipo.
Hata hivyo, ipo sababu moja kuu inayoweza kusababisha ucheleweshaji wa malipo kwa mwanachama, ambayo ni ukosefu wa nyaraka au taarifa muhimu zinazohitajika kutoka kwa mwanachama husika.
Kwa lengo la kutatua changamoto yoyote inayoweza kuwepo, Mfuko unatoa rai kwa mlalamikaji kupiga simu bure kupitia namba 0800 110040 ili kutupatia taarifa kamili za wahusika. Hii itatuwezesha kuchunguza suala hili kwa kina na kuhakikisha linashughulikiwa ipasavyo.
Mfuko wa PSSSF unajitahidi kila siku kutoa huduma bora kwa wanachama wake, na dhamira yetu ni kuhakikisha malalamiko au changamoto yoyote inatatuliwa haraka na kwa ufanisi.
Imetolewa na:
Yessaya Mwakifulefule
Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma