Nakushauri hata usifanye hiyo Test, hao jamaa wanao jiita Planet Action Fund, wanao tangaza ajira huko Sudani, Uganda na Congo ni matapeli, kwani hakuna NGO kama hiyo huko blackburn wala Preston wanakosema kuna ofisi zao.
Nina shawishika kuamini kuwa wana uhusiano wa moja kwa moja na hao wakenya wanao hiita TUMDA COMMUNICATION. Ili wapate dili ya hiyo PAAT.
Mini nilishatapeliwa 132,000 TSH. na hiyo PAAT test nilifanya lakini hamna kitu.
Kwa uhakika zaidi, hao Planet ACTION FUND. kwenye website hakuna maelezo ya kujitosheleza, lakini pia lugha yao imekosewa kosewa, lakini pia hawajatoa simu ya landline ya ofisi yao bali wametoa mobile number (tena lyca mobile)
kuweni makini na hawa jamaa, huu ni utapeli wa aina nyingine tena.