Zanzibar pia ni kituo kwa hiyo watachangia
Hata huko Dodoma na Dar wanaweza kuchangia pia, japo uwakilishi wao utakuwa mdogo..Zanzibar pia ni kituo kwa hiyo watachangia
Maoni ya watanganyika ndio yataamua hatima ya wazanzibari, hii inatokana na kweli ya kwamba vituo vimeweka Dodoma na Dar ktk ardhi ya Tanganyika.
Swali ni je wazanzibari watajifunza nini ? na je madai ya wazanzibari kutawaliwaliwa na mabeberu kutoka Tanganyika ni sahihi? na je ni hatua gani moja na ya uhakika wazanzibari wataichukua?
Kwani Mbeya, Kagera, Mtwara, Kigoma n.k watachangia lini?. Hii ni katiba ya Jamhuri ya Muungano na Zanzibar ni sehemu mojawapo tu ya Jamhuri kama mikoa mingine ya bara
Nimekuelewa. Mkuu.Ndio Mheshimiwa Nonda, nakubaliana nawe sikutaka kuandika mengi bali nilitaka kuleta hamasa kwa Wanzanzibar kuleta hoja zao hapa JF. Tatizo ni kwamba utaratibu mzima ni mbovu kupita kiasi, kuliwa na haja ya sehemu kubwa ya Jamhuri ya Muungano kushiriki lakini ccm kama kawaida yao hawataki ushiriki wa watanzania wengi. Kinachonishangaza zaidi ni kwamba Wazanzibar wako kimya mno kwa hili wala sijaona wakilalamika zaidi ya hii thread. Inaleta maswali mengi ya kujiuliza kwamba hivi baada ya CUF na CCM Zanzibar kufanya coaliation, Wazanzibar madai yao katika muungano ndio yamekufa? wanalidhishwa na hii hali ya muungano ndio maana CCM wanakiburi hata kuamua kuwa mambo ya muungano hayana mjadala katika mchakato wa katiba mpya unaoendelea?.
Wakuu zangu msianze kulalamika hovyo pasipo kuelewa maudhui ya Muswada wa Jk ambaye kasema wazi swala la Muungano lisiguswe..
Sasa la Wazanzibar wa nini ikiwa halitaguswa?
Kero yenu ni kero ya Watanzania wote na ndio maana sote tunaupinga muswada huu kwani hata bara tunataka nafasi yetu ktk Muungano ijadiliwe na hakika hakuna solution ila kwa kuunda serikali tatu na CCM hawawezi kukubali kugusa muungano ambao umewapa fursa ya kuunda serikali ya mseto kinyume cha katiba na taratibu za vyama vingi.
angalizo:
Kwa taarifa tu ni kuwa kamati ya bunge ya sheria na utawala ipo zanzibar asubuhi hii katika ukumbi wa bwawani na wadau mbali mbali wameshiriki katika mjadala huo. Punde tu nimetoka baada ya mkutano kuaikhirishwa hadi saa nane mchana baada ya salat el jumaa.