Pudding cake

Mrs Kharusy

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2013
Posts
1,244
Reaction score
671
Za jioni wapendwa!
Pishi la leo km jina linavyojieleza...samahani kwa wasiotumia sukari..

1) Katika suria ndogo kiasi weka sukari 5-6 tbsp. Yayusha kwenye moto mdogo mdogo huku ukiizungusha sufuria.
Wacha iyayuke yote iwe light brown iondoe kwenye moto na uisambaze pembezoni mwa sufuria.
Wacha sufuria ipoe.

Unga ngano 110gr
Siagi 120 gr
Sukar 100gr
Mayai matatu
Arki ya vanila
Cocoa vijiko 2
Baking powder 1/2 teaspoon

2) Kwenye bakuli safi Saga siagi na sukar kwa kutumia mashine ya cake.
Ikishasagika vizuri Weka mayai na usage tena.
Weka cocoa , vanila na BP..saga na uanze kuweka unga taratibu.
Weka mchanganyiko wako pembeni.

Mayai 8
Maziwa vikombe 4 (usitumie mug)
Sukari vijiko 6 (unaweza taste kupunguza au kuzidisha kiasi utachopenda)
Iliki 2 teaspoon
Arki 1tsp each (mimi naprefer banana+icecream)

3) Piga mayai na sukari kwenye bakuli safi hadi yachanganyike vizuri.
Weka maziwa kikombe kimoja kimoja huku ukiendelea kuchanganya vizuri.
Weka iliki na arki zako piga ichanganyike vizurii.

Chukua sufuria ulioiweka pembeni kwenye step 1.

Mimina mchanganyiko wa maziwa na mayai step 3.

Wacha itulie kidogo mimina mchanganyiko wa cake step 2..baada ya kumimina usiitikise sufuria, ifunike sufuria yenye mchanganyiko kwa foil vizuri uhakikishe mvuke hautatoka nje.

Chukua sufuria kubwa weka maji kiasi utumbukize sufuria yako yenye mchanganyiko taratibu usiitikise na uhakikishe haielei...km itaelea punguza maji kwenye sufuria kubwa.
Weka sufuria kubwa kwenye oven na uichome kwa 1 hr... In between uwe unaongeza maji kwenye sufuria kubwa ili yasikauke.. baada ya 1 hr fungua foil uweke kijiti kuiangalia km imewiva.
Nb. Kijiti kikitoka kikavu itakua imewiva. Itoe iwache hadi ipowe kabisaa.

Jinsi ya kuitoa kwenye sufuria:
Baada ya kupoa ondoa foil lizungushe zungushe sufua hadi uihisi imeachia pembezoni. Chukua sahani yenye ukubwa kuizidi sufuria yako yenye pudding cake yako ...birua kwenye sahani(km tunavyotengeza chips mayai). Weka kwenye fridge.
Pudding cake tayari kwa kuliwa.

farkhina Angel Nylon BAK mshana jr xiexie measkron King'asti Karucee ameline Swts gorgeousmimi Kim nana Ennie Jerrymsigwa Heaven on Earth ndetichia na wengine woote karibuni
 

Attachments

  • 1402511515619.jpg
    24.3 KB · Views: 979
Last edited by a moderator:
Maelezo ni marefu kwa wasiopenda kusoma km mimi ila upishi si mgumu ;-)
 
Ni easy tu kama pudding ya kawaida shoga si niweke na zabibu kavu itanoga eeeenh
 
Ntakuuliza maswal kama polisi lol.......enh hicho kipimo wanakula watu wangapi ntaka ku minimize

Usijali..Kwa ukubwa gani?..mm nakataga kidogo doogo ntapata hata vipiece 12
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…