Ndugu zangu,
Kuna wazo nakumbuka limekuwa likinisumbua siku nyingi. Watanzania kwa bahati mbaya, tukiwa mazingira fulani, tunapata taabu, wengine wanakuja kupita mazingira hayo hayo ambayo wengine tumepita, lakini cha ajabu tunashindwa kurudi kuwasaidia.
Kwa wale mliosoma Pugu, nakumbuka wakati mimi mnipo pale 1999-2001 tulikuwa na shida ya maji, tukaambiwa ni tatizo la muda mrefu. Likatutesa. Tukaliacha mpaka leo bado linaendelea.
Ombi langu wale waliosoma Pugu tuanzishe umoja wetu ambao kwa kuanzia tutaona namna ya kusaidia shule ile na pengine baadae kuwa na malengo makubwa zaidi.