PUGU Sekondari mmelogwa?

Gumilapua

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2011
Posts
855
Reaction score
591
Jana nilienda kumpeleka dogo, skuli ndio anaanza kidato cha tano! Kwenye inspection walikuwa wanakagua mambo kadhaa wa kadhaa. Vyote vilikuwa sawa ila kwenye upana wa suruali nadhani wanahitaji kujitafakari!

Walikuwa wanahitaji upana wa chini wa miguu uwe 20 inchi. Katika wanafunzi wote waliokuwepo wakati huo kama 13 hivi hakuna hata mmoja aliekuja na vipimo hivyo. Na hata waalimu na wazazi tuliokuja hakuna hata mmoja aliekuwa amevaa suruali yenye vipimo hivyo.

Mimi nadhani kuna haja ya kureview hitaji hili. Sijiwi ni nini kinachowasukuma kufanya hivi, au labda ni sehemu ya upigaji? Maana kuna mwl aliandaliwa ambae unamlipa tsh 2,000 kwa ajili ya kutanunua kila suruali.

All in all kuwavalisha watoto mabuga kama hayo sio fair, natoa wito kwa waalimu wawe wanaenda na wakati walau kidogo, inch 20 is too wide. Tuwatendee wenzetu vile ambavyo na sisi tungependa tutendewe.
 
Naona vijana wanazidi kuharibika kwa kuvaa vimodo na mentality itachange wakivaa suruali Pana ili kuleta nidhamu zaidi.
In my opinion 20 is too wide! I sent his picture in uniform, as day 1 at school to his brothers. Some of them commented on the pair of trousers being too big at the bottom, and that was before being taken for modifications by the teacher-tailor!
 
Hapo mbona wamepunguza mkuu,

Mimi nimesoma hapo walikuwa wanataka 22,wamechana sana suruali zangu jumatatu,ikabidi niwe nazo mbili,
Ya matukio na ya shule,

Jumatatu naruka na sare ya shule halafu siku nyingine napiga ya matukio,

Ila ya matukio usipite nayo sana jengo la utawala ITACHANWA.

kama unawezs atumie hyo mbinu
 
Anasoma DAY au BOARDING? Ni uniform tu, hakuambiwa na nguo zake za kawaida zifate mfumo huo....msije mkaanza na kusema, mtindo wa nywele n.k, 20inch haiathiri masomo yake sio? Avae tu hata kama ni Pepe Kale style.
 
Pole aisee. Sasa huyo dogo anashida gani hadi apelekewe shule?
Kuna baadhi ya shule wanafunzi kunyoa viduku ni ruksa.
Taratibu zingine za kijinga sana
 
Anasoma DAY au BOARDING? Ni uniform tu, hakuambiwa na nguo zake za kawaida zifate mfumo huo....msije mkaanza na kusema, mtindo wa nywele n.k, 20inch haiathiri masomo yake sio? Avae tu hata kama ni Pepe Kale style.
Ameenda boarding, sasa najiuliza zile siku za outing sijui wanatokaje na hizo uniform, huko mtaani si watu wanakuona kama kituko?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…