Naenda moja kwa moja kwenye mada. Jana nimepita kujaza mafuta kwenye kituo kimoja sitakitaja nimefurahishwa sana na uelewa aliokuwa nao pump attendant aliyekuwa ananihudumia, ni hivi nilipofika pale nimesimamisha gari akaniamrisha nizime gari nikazima lakini nikasema ngoja nimhoji ni kwanini ananilazimisha kuzima gari akanielimisha sababu mbili.
1. Ni kwamba kwakuwa wakati wa kujaza mafuta mvuke wa mafuta unakuwa umetapakaa hivyo kikipatikana chanzo chochote kama cheche inaweza kusababisha moto.
2. Ni kwamba mafuta yanapoingia kwenye gari uingia kwenye tank kwa kasi hivyo hutibua uchafu uliopo kwenye tank la gari sasa gari inapokuwa on kuna uwezekano mkubwa pump ya gari ikavuta uchafu kupeleka kwenye injini na ni kweli matank ya magari uwa na uchafu na sijui unatokeaga wapi.
Kwa hili nikaona ni vizuri hawa Pump Attendant wakapata mafunzo kwa maana wanakutana na wenye hivi vyombo kwa wingi na watatoa elimu iliyobora.