Hongereni sana kwa wale mnaotaka kujiunga na Kilimo cha umwagiliaji....Mimi sina utaalam sana ila naweza nikachangia kitu kwenye hii mada...jaribu kupitia hizi pump below..ni nzuri sana
1.WT40XK3C...Honda trash pump kama shamba lako ni kubwa...4inch
2.Honda WT30XK4C...3inch
3.Honda WH20X high pressure water pump...2inch
4. Honda WB30...3inch
hizo pump kuna ya 4m hadi ya 1m..hizo ndo pump nzuri kwa mashamba ya kuanzia ekari tano..Mashamba yanamwagiliwa kwa mifereji..yaani unakuwa na point moja(center) ambapo utakuwa unapump hayo maji, afu from there unayasafirisha kwa mfereji..hiyo point jitahidi iwe katikati au sehemu yenye muinuko zaidi katika shamba lako..
Unaweza kuzipata hizo pump kwenye duka la Honda lililopo kariakoo, lipo karibu na zilipokuwa ofisi za scandnavia..
Kumbuka, kama unataka kufanya kilimo cha umwagiliaji kitu cha kwanza muhimu ni ubora wa pump..nakushauri achana na pump za kichina kama pesa yako ni yakuunga unga maana zinahitaji maintenance za mara kwa mara...they look cheap but they r expensive...
Ukiweza pata pump za Diesel ni much better