Ni mwaka sasa umetimia tar kama ya leo 28/3/2011 nilipoondokewa na wewe mwanangu kipenzi IKUPA MWAKYUSA (14yrs) pale Lugalo hosp,najua ulilala tu na sasa umevikwa mwili mpya usiokufa ukipumzika mahali pema peponi.msg to jf bros.
Pole sana mkuu Michael wewe na familia yako.
Uchungu wa kumpoteza mwana ni mzazi tu
anaufahamu. Tungependa kuungana nawe
kwa siku hii ya kumbukumbu. Mwenyenzi Mungu
Azidi kumlinda malaika wake Ikupa.
AMEN.
Mkuu pole sana,bahati mbaya bishanga ni maimuna wa kompyuta na hivyo naomba uniunganishe na mimi katika kadi aliyokutumia Afrodenzi hapo juu.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya mwanetu,Ameen.
Pole sana mkuu,tutakutana siku ya mwisho tukiwa tumevaa mwili mpya lakini kwa wale wateule.Cha msingi tuyaishi maisha yanayompendeza mungu,tutonana tu siku ya mwisho.Pole tena mkuu
Pole sana Michael. Tushukuru kwa kila jambo. bali kibinadamu ni ngumu sana hadi kwa msaada wa Mungu.
Ni malaika na yupo mbinguni sasa akiimba na kusifu pamoja na malaika kama ilivyoandikwa.
Mungu akupe faraja ya milele itokayo kwake.