TANZIA Pumzika kwa amani Profesa Costa Ricky Mahalu!

Ahukumiwe anavyostahili. Haya majitu yalifikiria kujitajirisha tu! Let him face the real justice and democracy!
 
Balozi Profesa Costa Ricky Mahalu amefariki dunia mchana wa leo, Machi 9, 2026, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu akiwa na umri wa miaka 77.

Hizi hapa ni baadhi ya hatua muhimu katika maisha na kazi yake:
Wasifu na Kazi ya Diplomasia
Kuzaliwa: Alizaliwa Julai 9, 1948, katika Kijiji cha Katunguru, Wilaya ya Sengerema.

Balozi wa Italia: Alihudumu kama Balozi wa Tanzania nchini Italia (makazi yakiwa Roma) kuanzia mwaka 2000 hadi 2006. Pia aliwakilisha Tanzania katika mashirika ya kimataifa kama FAO, WFP, na IFAD
Kurejeshewa Hadhi ya Ubalozi: Mwaka 2018, aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Magufuli, alimrejeshea rasmi hadhi yake ya ubalozi baada ya kukutwa hana hatia katika kesi ya matumizi mabaya ya ofisi iliyokuwa ikimkabili tangu mwaka 2007.

Taaluma na Elimu
Makamu Mkuu wa Chuo (VC): Hadi kifo chake, alikuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT) kuanzia Machi 1, 2019.

Mwanasheria Nguli: Alikuwa Profesa wa Sheria na mwanasheria wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Alijulikana sana kwa utaalamu wake katika Sheria ya Kimataifa ya Majini (Maritime International Law).

Elimu: Alipata Shahada yake ya kwanza na ya pili ya Sheria (LLB & LLM) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Chuo Kikuu cha Hamburg, Ujerumani, mwaka 1983.

Michango Mingine Kitaifa
Bunge la Katiba: Mwaka 2014, aliteuliwa kuwa mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba na aliongoza kamati iliyoandaa kanuni za bunge hilo.

Elimu ya Juu: Alihudumu kama Mkurugenzi wa Elimu ya Juu nchini (1992–1996), ambapo alishiriki katika mchakato wa kuruhusu vyuo vikuu binafsi na kuanzishwa kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).
 
Ulikuwa unapiga Nyeto?! Taarifa ndio zinakufikia muda huu?!
Mkuu kwamba hatuna shughuli ni kushinda Mtandaoni Tu?!

Pia hata kama habari uliifahamu muda mrefu mbona hukuweka jukwaani kuufahamisha umma mpana zaidi?
Binafsi nimeona humu jukwaani habari haijawekwa ndio nikapost
By the way ahsante Kwa luhha yako chafu
 
Baada ya sekunde 30 uzi wako utaunganishwa na post mama
 
Kuna mwamba mwingine anaitwa Mahalu, at one time alikuwa Cuhas Bugando, wana undugu?
Kuna mwamba mwingine anaitwa Mahalu, at one time alikuwa Cuhas Bugando, wana undugu?
 
Thanks for this, nimeisoma The Citizen, Tanzania mourns renowned academic and diplomat Prof Mahalu

Prof. Mahalu, namkubali sana!
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…