TANZIA Pumzika kwa amani Said Makilagi, mfanyabiashara mkubwa wa nafaka na mmiliki wa Musoma Food

TANZIA Pumzika kwa amani Said Makilagi, mfanyabiashara mkubwa wa nafaka na mmiliki wa Musoma Food

mockers

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2013
Posts
12,843
Reaction score
35,442
Maneno sio mengi sana.

Napenda kutoa pole za dhati kwa familia kwanza ya Musoma Food, ndugu, jamaa na marafiki, kwa kumpoteza mfanyabiashara huyu mkubwa wa nafaka kanda ya ziwa na pengine Tanzania.

Pole ziwafikie pia wafanyakazi wa kampuni ya Musoma Food kwa kuondokewa na bosi wenu ambae aliishi nanyi kama familia.

Hakika ni msiba mkubwa sana kuanzia kote alikokuwa akinunua mazao ikiwamo nchi za Zambia, Uganda, na mikoa karibu yote Tanzania, maana kampuni ilikuwa inafika bei bila tatizo hata kulipotokea ushindani wa wanunuzi wa nje bado alitoa bei nzuri sana ya mazao kama mpunga, mahindi, mtama na kadhalika.

Pumzika kwa amani Side.

R.I.P
 
Maneno sio mengi sana.
Napenda kutoa pole za dhati kwa Familia kwanza ya Musoma Food, Ndugu, jamaa na marafiki, kwa kumpoteza mfanyabiashara huyu mkubwa wa nafaka kanda ya ziwa na pengine Tanzania,
Pole ziwafikie pia wafanyakazi wa kampuni ya Musoma Food kwa kuondokewa na Bosi wenu ambae aliishi nanyi kama familia.
Hakika ni msiba mkubwa sana kuanzia kote alikokua akinunua mazao ikiwamo nchi za Zambia, Uganda, na Mikoa karibu yote Tanzania maana kampuni ilikua inafika bei bila tatizo hata kulipotokea ushindani wa wanunuzi wa nje bado alitoa bei nzuri sana ya mazao kama mpunga, mahindi, mtama na kadhalika.
Pumzika kwa amani Side,
R.I.P
makilagi sio jina geni
 
makilagi sio jina geni

Ni mfanyabiashara mkubwa wa nafaka na bilionea ambaye alipata tenda za kusambaza mchele, unga, maharagwe kwenye kambi za wakimbizi kuanzia Tanzania, Sudani, Congo kwa miaka mingi amekua akifanya kazi na WFP, kwa mtu wa mazao yeyote Tanzania lazima umfahamu huyu mwamba, wa Musoma Food aliejikita Shinyanga kulipo na viwanda vyake
 
Maneno sio mengi sana.
Napenda kutoa pole za dhati kwa Familia kwanza ya Musoma Food, Ndugu, jamaa na marafiki, kwa kumpoteza mfanyabiashara huyu mkubwa wa nafaka kanda ya ziwa na pengine Tanzania,
Pole ziwafikie pia wafanyakazi wa kampuni ya Musoma Food kwa kuondokewa na Bosi wenu ambae aliishi nanyi kama familia.
Hakika ni msiba mkubwa sana kuanzia kote alikokua akinunua mazao ikiwamo nchi za Zambia, Uganda, na Mikoa karibu yote Tanzania maana kampuni ilikua inafika bei bila tatizo hata kulipotokea ushindani wa wanunuzi wa nje bado alitoa bei nzuri sana ya mazao kama mpunga, mahindi, mtama na kadhalika.
Pumzika kwa amani Side,
R.I.P

Kumbe musoma food ilikuwa yake, nilidhani ya Matayo.
 
RIP Bilionea Makilagi

Mazishi ya msiba wa Said Kate Makilagi wa Musoma Food, vilio mjini Shinyanga

Maelfu ya waombolezaji wamejitokeza kuaga mwili wa Mfanyabiashara wa nafaka mkoa wa Shinyanga Said Makilagi maarufu Musoma Food aliyefariki dunia ghafla jijini Mwanza Jumatatu Aprili 3,2023 akiwa Hotelini.

Mazishi ya marehemu Said Kate Makilagi yamefanyika leo Alhamisi Aprili 6,2023 nyumbani kwake Kambarage Mjini Shinyanga.

Kwa mujibu wa taarifa ya familia tarehe 27.5.2021 Said Makilagi alipata ajali ya gari huko Mpanda Rukwa akapelekwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa ajili ya matibabu na kutokana na afya yake kutetereka alikuwa akipatwa matibabu Bugando, Kenya na India.

Hata hivyo kutokana na matibabu hayo alipata nafuu na kwa nyakati tofauti alikuwa anapata maumivu ya kichwa na mnamo tarehe 3.4.2023 akiwa jijini Mwanza aliugua ghafla jijini akafariki dunia.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Musoma Food, Said Kate Makilagi alizaliwa 01.06.1967 alifariki dunia 03.04.2023, ameacha mjane na watoto wawili

Salaam za rambirambi zamiminika toka kila kona ya nchi zimetolewa, Bwana Alitoa na Bwana Ametwa jina lake lihimidiwe

1680959496629.png

RIP Bilionea Makilagi

Mazishi ya msiba wa Makilagi wa Musoma Food, vilio mjini Shinyanga

Kabisa Musoma kwao, na shinyanga kwake ambapo alifanyia uwekezaji mkubwa ni vilio vikubwa lakini ni vilio sehemu mbalimbali Ndani na nje ya nchi
 
NAHISI ALIKUWA NA WATOTO WANENE HIVI NA PIA ALIKUWA NA MAZIWA YANAITWA MAKILAGI HADI WAMAMA WA TARIME WENYE MAZIWA MAKUBWA WAKAWA WANAITWA MAKILAGI.
 
NAHISI ALIKUWA NA WATOTO WANENE HIVI NA PIA ALIKUWA NA MAZIWA YANAITWA MAKILAGI HADI WAMAMA WA TARIME WENYE MAZIWA MAKUBWA WAKAWA WANAITWA MAKILAGI.

Yule alikua ndugu yake, yeye said aliuza hadi simu miaka ile zinaanza kuingia Tanzania na the rest ikawa story
 
Back
Top Bottom