Hawa watu wamezidiana vitu kadhaa naomba nikufafanulie.na kumchanganua mmoja mmoja.
Evander Holyfield - huyu ni mmoja ya mabondia wenye endurance kubwa,sugu au uvumilivu wa kupokea kipigo.huyu ni jamaa ambaye unaweza ukapiga mpaka ukachoka.utapiga anakufuata naye anakupiga,utapiga anakufuata naye anakupiga.na hili lilimpa shida sana tyson kumshinda evander.ngumi zake zilikuwa kali lakini si za kutisha sana.na alikuwa mtu ambaye hachoki kirahisi.
Mike Tyson - huyu alikuwa na nguvu na speed/kasi.alikuwa na ngumi zenye nguvu sana na uwezo wa kuhama alipo au kukufuata kwa kasi huku akirusha ngumi zenye uzito.na hii inatokana na namna ya kurusha kwake ngumi.ngumi yake ilikuwa inakuja na uzito wa mwili wake pia.ila hakuwa na uwezo wa kupokea sana kipigo,hakuwa na pumzi sana kama evander holyfield.ndo maana ilikuwa tyson ukishamvusha round ya 5 ukaenda naye ya 6 tayari ana panic maana hakuzoea kwenda rounds nyingi hivyo hakuwa na pumzi na pia kisaikolojia alikuwa anaathirika.
Lennox Lewis - this man alitumia zaidi akili na urefu wake kwa advantage.alikua anajua namna ya kumchosha adui yake.naye hakuwa mvumilivu sana kwenye kipigo.alikosa ile spirit ya evander holyfield.alipigana kwa akili kumchosha mpinzani na pia alikuwa na ngumi zenye uzito mzuri.
So kwa ngumi kali ntasema alikuwa Mike Tyson. Ila Mambo mengine hao jamaa kama ambavyo nmeelezea. Mimi nlimpenda Evander sababu ya Usugu wake na alipotokea hakuwa anadhaniwa angefika pale hasa kiafya kutokana na kuwa na mwili mdogo ingawa mrefu.