MALKIA WA TABASAMU
Member
- May 23, 2024
- 15
- 43
Tunaumizwa na watu tunaowapenda. Tumewapa haki hiyo tulipojiaminisha upendo tulionao kwao ndio walionao kwetu. Tumechagua wenyewe kuumia.
Haki ya kulibangua hilo na kuliweka kwenye kipimo stahiki imeshikamana sana na mataraja yetu. Tunaamini tunavyovitarajia kuliko vilivyobwagwa upeoni mwetu.
Nikiweka asilimia kwenye mahusiano, matarajio ya mwanaume kuhusu kubadilika kwa baadhi ya tabia za mwanamke huwa haizidi asilimia 20.
Mzani huo ukitumika kupima matarajio ya mwanamke juu ya mwanaume aliyemridhia kubadilika kitabia haipungui asilimia 80.
Mwanaume anaweza kumuoa mwanamke mwenye tabia mbaya anayomudu kuivumilia.
Mwanamke anaweza kuolewa na mwanaume mwenye tabia asizoweza kuzivumilia kwa kigezo cha kutarajia tu mabadiliko.
Kwenye kitabu cha MWANAMKE WA THAMANI NDANI YANGU nimeliandika hili vizuri sana.
WATU HUBADILIKA WAKIAMUA NA SIO KWA SABABU WEWE ULITAKA/ULITARAJIA WATABADILIKA.
Swali muhimu unalopaswa kujiulizq kabla ya kuingia kwenye agano la kudumu na huyo mtu umpendaye sana, je! tabia zake korofi utazimudu?
Usijipe matarajio ya yeye kubadilika. Nakuambia hili kwa sababu watu wengi sana wakishapata kile cheti husahau kabisa kuongeza bidii ili wakuze viwango na maksi zao ndani ya NDOA.
Kabla hamjatia saini kwenye hivyo vyeti, hakikisheni matarajio ni madogo na uhalisia ni mkubwa.
Kila mmoja apime nguvu yake kwenye kumudu haswa madhaifu ya kitabia ya mwenzake. Ukiona nguvu ni ndogo, lijimtabia ni likubwa..... JIPE MUDA.
Maisha yanaweza kuanza muda wowote utakaoamua kuyaanza ukiwa na mtazamo chanya wa mambo na watu.
Ikiwa ni kijana, wekeza kwenye kupata maarifa. Kuna mambo ningeambiwa miaka kumi iliyopita, kuna makosa nisingefanya asilani.
Japokuwa makosa niliyoyafanya, yamenifinyanga na kunipa ujasiri nilionao leo, kuna baadhi ya madoa hayafutiki kirahisi nakwambia. Ni mimi nilipewa nguvu hiyo, pengine shauri ya wito huu wa uelimishaji, jiulize, ukibugi kwenye 20's yako utakuwa na ujasiri huu kwenye 30's au 40's huko? Usitengeneze mazingira ya kuja kulaumu watu huko utu uzimani hali ya kuwa unaweza kupanga sasa hivi.
Kumbuka....
MAKOSA WALIYOYAFANYA WENGINE YAKAWAJENGA, YANAWEZA KAKUBOMOA WEWE KWA KUYAJARIBU TU.
Fanya shingo yako iwe laini. Panapofaa kugeuka fanya hima mapema. Muda haumngoji yoyote kati yetu.
Mungu atusaidie.
✍ Malkia wa tabasamu.
Kungwi wa kisasa.