Sometimes mtoto anahitaji mwongozo toka kwa wazazi/walezi. Utakuta wengine wanao uwezo darasani lakini hawana uelewa wa masomo gani wachukue. Hapo walezi wana nafasi ya kuongea nae na kumwelekeza. Mazingira pia yanachangia. Mfano mtoto wa kijijini ukimwambia unataka uwe nani? majibu yake lazima yatatofautiana na mtoto wa mjini,kwahiyo mlezi/mzazi hana budi kumwelekeza kama yeye mwenyewe pia kasoma na kupitia life tofuatitofauti. Anaweza kumpa experience yake kuhusu masuala ya masomo na career development. Lakini sio ile mtoto hawezi hesabu wewe unamlazimisha asome hesabu ili aje kua Computer geek...hiyo sio,utachemsha tu.!
...naaam, naaam!
Mtoto wa Kijijini huenda akataka kuwa Mwalimu, kwani ndiye pekee anayeonekana ana hadhi ya kujivunia kwenye jamii...
Lakini cha ajabu, mawaziri, makatibu wakuu, wakurugenzi, na Mabalozi wetu na wengineo wengi walizaliwa huko mikoani, wengine vijijini kabisa miaka hiyo.... wengi wao baada ya Tabora school enzi hizo nk... walipitia Makerere na kuendelea kwenye vyuo vikuu nchi mbali mbali duniani na kuishia kufanya kazi za kimataifa i.e Udakitari, nk...
Who pushed them? Mkoloni? jamii ilomzunguka? au juhudi binafsi?
Leo hii unamgharamikia mwanao kuanzia Chekechea, unamlipia primary na secondary education kwenye Academies, lengo lako ni kumpa elimu tu bila matarajio yeyote akishamaliza?
au, Una experience gani binafsi wazazi wako
walivyokusukuma kielimu kufikia malengo yao?
Binafsi, ningesikiliza matakwa ya jamii ilokuwa inanizunguka, huenda ningekuwa Dakitari kama ilivyo asilimia kubwa ya ukoo wangu.