Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Baada ya shambulio kali la Urusi kuua idadi kubwa ya askari kuruta wa Ukraine kwenye jimbo la Donest,leo raisi Putin wa Urusi ameweka wazi kuwa wamekuwa wakisonga mbele kwa kasi kuelekea kushika miji muhimu ya Donbas kutokana na kutokuwepo kwa upinzani wa askari wa Ukraine.
Wiki tatu zilizopita vikosi vya Ukraine vyenye mafunzo ya hali ya juu vilivuka mpaka kuingia eneo la Urusi la Kursk na kutangaza kuwa wameweza kuteka zaidi ya kilomita za mraba 1000.Jambo la kushangaza ni kwamba jeshi la Urusi tangu siku hiyo halijatumia nguvu kubwa kuwatoa askari hao kutoka ndani ya mipaka yake.
Soma Pia: Ukraine yateka vitongoji vya Urusi kwenye jimbo la Kursk
Shambulio la juzi huko kwenye shule ya kijeshi ya Polvosk limeaacha majonzi makubwa kwa serikali yenyewe na wazazi wa vijana hao wadogo waliokuwa wakipata mafunzo.Wengi wa wazazi hao wamekataa kusifia vikosi vya Ukraine kuingia Kursk kwani mafanikio hayo yamekuwa ni madogo kuliko hasara iliyopatikan upande wao. Ni afadhali askari wao wangebaki nyumbani ili kuwalinda watoto na wao wenyewe.