Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Pwani kimeanza kwa kasi utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa ofisi ya chama hicho, ambao sasa uko katika hatua za msingi na unaendelea vizuri.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi, Baraka Nandonde, amethibitisha kuwa mafundi wameshaingia eneo la mradi lililopo Mathias, wilayani Kibaha, na kazi inaendelea.
Nandonde amesema ujenzi upo katika hatua ya msingi na kila kitu kinaenda vizuri. Alisisitiza kuwa kamati yao inatarajia ofisi hiyo izinduliwe na Mwenyekiti mpya wa Taifa atakayechaguliwa katika uchaguzi mkuu wa chama unaotarajiwa mwakani.
Nandonde ametoa wito kwa wanachama na wadau wa chama kushirikiana ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa mafanikio, akiongeza kuwa ofisi hiyo itakuwa ni kitovu cha kuimarisha utendaji wa chama katika Mkoa wa Pwani.
Chanzo: Jambo TV