Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mbio hizo zenye jina la Coast City Marathon zinalenga pia kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukizwa, kuibua vipaji vya wanariadha pamoja na kuimarisha Utamaduni wa Jamii kuchangia shughuli za Maendeleo.
Mkuu wa Idara ya Elimu Awali na Msingi ndiye aliyekuwa Mgeni Maalum akimwakilisha Mkurugenzi wa Mji Kibaha Dkt. Rogers Jacob Shemwelekwa amefurahishwa na Maandalizi hayo pamoja na malengo yake kwani yanakwenda kuunga Mkono Juhudi za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za uwekezaji kwenye Sekta za Elimu na afya za watu hususan kwenye mapambano dhidi ya maradhi yasiyoambukiza.
Afisa Michezo wa Halmashauri ya Mji Kibaha amebainisha kuwa kutakuwa na mbio za Kilomita 2.5 mahusus kwa Watoto, Kilomita 5 za Veterani na watu wenye umri mkubwa na Kilomita 10 na 21 zitakuwa kwa ajili ya wakimbiaji wazoefu, ambapo zawadi zitatolewa kwa mshindi wa 1-3
Dkt. Mhambwa amewashukuru wadhamini wote kwa kufanikisha mbio hizo ambazo zitaanzia na kuishia kwenye bustani ya Michezo iliyopo Mailimoja.
Coast City Marathon Mwaka 2023 ilihusisha wakimbiaji zaidi ya 500, hivyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi Dkt. Frank Mhambwa ametoa rai kwa wote wenye afya njema kushiriki kwa kuchangia Tshs. 35,000/= ili zikatekeleze lengo lililokusudiwa.