Pwani: Madai ya Halmashauri kuingia Mitini na 150,000 za Wananchi, Mwenyekiti wa Mtaa afafanua

Pwani: Madai ya Halmashauri kuingia Mitini na 150,000 za Wananchi, Mwenyekiti wa Mtaa afafanua

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kueleza kuwa Serikali ya Mtaa ya Muheza pamoja na Halmashauri ziliwatoza Wananchi wa maeneo hayo kiasi cha Tsh. 150,000 kwa ajili ya kupimiwa ardhi kuanzia Mwaka 2020 lakini hakuna kilichoendelea, ufafanuzi umetolewa.

Kumsoma Mdau, bofya hapa ~ Wakazi wa Muheza, Maili Moja – Kibaha tulilipa Tsh. 150,000 tupimiwe Viwanja, huu Mwaka wa 4 kimyaaa

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Muheza, Jackson Mwile amezungumza na JamiiForums.com na kutoa ufafanuzi:

Anasema “Ni kweli hela walilipa, walilipa kupitia Halmashuri ya Kibaha, walifanya zoezi hilo baada ya Wananchi kulipa, ambao bado hawajapimiwa unakuta hawakuwepo wakati wa zoezi hilo.

Zoezi lilikuwa linafanyika wakati wamiliki wanapokuwa maeneo husika, wle ambao hawakuwepo walituma wawakilishi walirukwa kwa kuwa lolote linaweza kutokea na wakawaruka wamiliki kisha ikawa tatizo.

Anasema “Unakuta mtu anasema pimeni hapo yupo Mfanyakazi wake, hili lilikuwa halikubaliki, inawezekana hata huyo mlalamikaji labda naye hakuwepo wakati upimaji unafanyika.

“Hakuna mtu ambaye amedhulumiwa, wasiopandiwa mawe wapo 10, ambao wamepandiwa mawe lakini hayajaingizwa kwenye GPS wapo 9, wasiochukua mawe wapo 17, waliolipia mawe na kukamilisha mchakato wa kupata Hati jumla ni 184.

“Ukitaka kwenda kupima mwenyewe peke yako unaenda kulipia Milioni 1.5, kwa kuwa wenye uhitaji ni wengi Halmashauri ikaamua iwafanyie unafuu kwa kutoa Sh 150,000.”
 
Back
Top Bottom