Pre GE2025 Pwani: Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete aboresha taarifa zake kwenye daftari la kudumu la mpiga kura

Pre GE2025 Pwani: Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete aboresha taarifa zake kwenye daftari la kudumu la mpiga kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Mbunge wa Jimbo la Chalinze na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe Ridhiwani Kikwete Jana amejitokeza katika Ofisi ya Kata ya Msoga kwa ajili ya kujiandikisha na kuboresha taarifa zake katika Daftari la kudumu la Mpiga kura ili aweze kupata fursa ya kuchagua viongozi kwenye uchaguzi.

Kikwete ametumia fursa hiyo pia kuhamasisha wananchi wengine kujitokeza kujiandikisha au kuboresha taarifa zao ili haki hii muhimu ya kupiga kura isiwapite. Zoezi hili limeanza tarehe 13 Februari na litaisha Februari 19, 2025 kwa mkoa wa Pwani na Tanga na hivyo kuwataka wananchi kutumia fursa hii kwa siku hizi.

Soma pia: Ummy Mwalimu awahimiza wakazi wa Tanga kwenda kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura


Snapinst.app_480091902_18489087229044218_1631186412655140644_n_1080.jpg




Snapinst.app_479923684_18489087265044218_5786301047463761634_n_1080.jpg
 
Back
Top Bottom