Uchaguzi 2020 Pwani: Mgombea Urais wa ADC, Queen Cuthbert Sendiga asema inatia huruma Mkulima kutegemea jembe la mkono kubadilisha maisha

Uchaguzi 2020 Pwani: Mgombea Urais wa ADC, Queen Cuthbert Sendiga asema inatia huruma Mkulima kutegemea jembe la mkono kubadilisha maisha

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Queen Cuthbert Sendiga ameendelea leo na Kampeni zake baada ya siku tatu za mapumziko ambazo alizitumia kufanya media tour jijini Dar es Salaam.

Akiwa katika Mkoa wa Pwani wilaya ya Kisarawe, aliweza kukutana na makundi mbalimbali na kuweza kunadi sera zake huku akitilia mkazo sera ya kilimo.

"Mkulima wa sasa bado anatumia jembe la mkono na anategemea kubadilisha maisha yake hili ni jambo la kutia huruma sana. Mkulima wa sasa anahitaji uhakika wa nyenzo bora za kulima, pembejeo za kisasa, uhakika wa kuuuza mazao yake akishakua amevuna, hii yote naenda kuitilia mkazo katika muda wangu wa kuwa madarakani endapo mtanipatia kura ya ndio tarehe 28 mwezi huu"

Mgombea ataendelea na Kampeni zake kesho Jumamosi katika wilaya ya Bagamoyo na kuendelea na kampeni zake kusini mwa nchi.
IMG_20201002_205241_067.jpg
IMG_20201002_205238_040.jpg
IMG_20201002_205234_596.jpg
IMG_20201002_205230_172.jpg
IMG_20201002_205226_515.jpg
IMG_20201002_205223_052.jpg
IMG_20201002_205220_520.jpg
IMG_20201002_205215_571.jpg
 
Siku hizi huyo mwanamke yuko wapi?
Hawakumfikiria hata uongozi
 
Back
Top Bottom